The House of Favourite Newspapers

TP Mazembe yavunja rekodi ya Yanga

0

YANGA VS TP MAZEMBE (9)Omary Mdose na Nicodemus Jonas

USHINDI iliyoupata TP Mazembe ya DR Congo dhidi ya Yanga, Jumanne ya wiki hii, umevunja rekodi ya Yanga ya kutofungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa takribani miaka sita iliyopita katika michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa Kundi A katika Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa kundi moja na timu nyingine za Medeama ya Ghana na MO Bejaia ya Algeria.

Rekodi zinaonyesha kuwa, mara ya mwisho Yanga kufungwa nyumbani katika michuano hiyo na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa ni mwaka 2010 ambapo ulikuwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu ya Saint Eloi Lupopo ya DR Congo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar, Yanga ilifungwa mabao 3-2, mchezo wa pili nchini DR Congo, Yanga ikafungwa tena bao 1-0.

Yanga ipo chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye ana uwezo mkubwa wa kifedha wakati Mazembe inamilikiwa na Moise Katumbi ambaye naye ni mmoja wa matajiri wa DR Congo.

 

Leave A Reply