The House of Favourite Newspapers

Simulizi ya Msamaha wa Mama – 11

global-instaRiwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 11

Profesa Sharif aliongea jasho tayari likiwa linamwagika usoni mwake, alikuwa amevaa miwani midogo ya duwara ilibidi aivue baada ya kuona kama haoni vizuri, Upara wake ulianza kuloana loana jasho japo A/C ilikuwa inapuliza.

Nini kiliendelea?…
Songa nayo….

Mzee shaibu aliiona hali ya profesa kubadilika, Alimuangalia na kumuacha kama alivyo.
” Kiukweli Sina la kusema mzee wangu zaid ya kukubali tuhuma, ila naomba hizi habari zisifike kokote, nakuomba sana mzee wangu. Aliongea sharif katika hali ya woga.

” Ni nani aliefanya hizi mbinu zote za kukushawishi wewe hadi ukauza matokeo na kakupa kiasi gani ambacho serikali haikupi?. Alimuuliza akiwa ameegamia vizuri kiti alichokuwa amekalia.

” Mr Zubeir. Alisema kumjibu swali lake.
Mzee shaib alitoa macho ya mshtuko baada ya kutajiwa hilo jina, Mr zubeir ni mtu aliekuwa anamfahamu vizuri kwa utajiri alionao ndani na nje ya Zanzibar.
” Ndie huyo mzee wangu, mwanae kafeli akanambia nimpatie matokeo mazuri ya kufaulu atanipatia pesa mara mbili ya nnayolipwa na Serikali, ikabidi niuze ya seid kwa sababu ndio mwanafunzi pekee aliekuwa akisoma green school kwa msaada wa waziri baada ya matokeo yake kuwa mazuri kuanzia kidato cha nne na kidato cha tano.

Mzee shaibu aliachia pumzi ya kuchoka, hakuwa na la kuongea lengine zaidi ya kumuomba abadilishe matokeo ya kijana, mwisho alitoka ofisini akisema
“Nakupa masaa mawili matokeo yawe sawa laa sivyo unaumbuka.
” Sasa hivi nafanya hivyo ila naomba sana hizo habari zisifike kokote. Alisema sharif akimuangalia mzee shaib.
” Usijali Profesa endelea na kazi yako.

Alitoka nje ya ofisi akakutana na baadhi ya maprofesa wadogo wadogo, aliwaaga na kuanza kutoka nje kundoka.
Sharif ndani alibaki presha juu juu huku akijilaumu kwa mambo aliyoyafanya akijua anajitengenezea maisha bila kujua kuwa anaharibu.

Seid na hamad muda wote walikuwa wamekaa kwenye gari wakiongea baadhi ya mambo hasa kuhusu ticha, Mzee shaibu aliingia moja kwa moja katika gari lake, Hamad alimuona baba yake kipindi anatoka ofisini na kujua hayuko sawa, akiwa anataka kushuka katika gari kwenda kumuona, Tayari baba yake akawa ameingia kwenye gari, magari yakaanza kutoka kuelekea sehemu nyingine.

Hamad nae aliwasha gari haraka akaufata msafara wa magari matano ambao gari la nyuma kabisa lilikuwa na wazee wa kutuliza ghasia FFU.
“Mbona anaenda huku vipi?. Seid alimuuliza rafiki yake baada ya kuona magari yanaelekea bara bara tofauti na ya mjini ambapo kuna makazi yao.
” Sisi tufate tu kwa sababu hata mimi sijui. Ghafla cm ya hamad ilianza kuita, aliitoa mfukoni na kuangalia anaepiga akakuta my Fatha, alipokea na kuweka sikioni.

” Ndio baba.
” Tunaenda kwa waziri wa Elimu, mumenifata kwa nyuma!?
” Ndio, tuko nyuma.
” Ok

Cm ilikatwa hamad yake akaiweka pembeni ya mfuko wake, Mzee Shaibu baada ya kukata aliingia upande wa majina na kumpigia mkewe, baada ya kupokea alimuambia aende ofisini achukue baadhi ya vifaa vyake, yeye atachelewa kurudi kuna swala analishugulikia kisha kukata.

” Vipi?. Seid alimuuliza rafiki yake .
” Kasema tunaenda kwa waziri wa Elimu, na bora twende maana na mimi kulikuwa na vitu flan navitaka kutoka kwake.
” hajakwambia kufanya nini.
” hajanambia twende tu, nadhani kutakuwa kuna jambo tayari limefahamika.

Walienda mpaka katika ofisi ya waziri wa elimu ilioko karibu na police k/samaki. Walipofika mzee shaibu aliingia ndani kwenda kuonana nae.

Secretal wa waziri alishangaa sana kumuona mzee huyo yuko mbele yake, walisalimiana na kuongea mawili matatu kwa sababu walikuwa wamezoeana, kisha akaruhusiwa kuingia ndani kwa Waziri baada ya kuuliza na kuambiwa yupo ndani.

Waziri sura yake ilijawa na tabasam la furaha alipomuona mzee shaibu, alinyanyuka katika kiti chake akatoka upande wa pili wa meza, ambapo alikutana na mzee shaibu wakakumbatiana huku wakicheka kwa furaha.
” Za siku nyingi bhanaaaa, Upoooo, umepotea mzee mwenzangu, ,, karibuuu sana. Hahahaaa
Yalikuwa maneno ya waziri akiyaongea kwa furaha huku mzee shaibu akiyaitikia yote. mwisho alikaa kwenye kiti, Waziri nae alizunguka kwenda kwenye kiti chake huku akisema.
” Leo sikutarajia kupata ugeni mkubwa kama huu, Kabbisa kabisa vipi nyumbani wanasemaje?.
” Hawajambo, Vipi hali?
” Aisseee hapa tunamshukuru Mungu, kwanza kabisa kabla ya yote, nipatie namba ya kijana wako, yuleee! nani nani!!.
“Hamad! ,, Mzee shaibu alidakia kumkumbusha alipoona anatafuta jina halipati.
” Eheeeeeee! mi napenda sana kumuita kichwa, pale mzee mwenzangu umezaa, mtoto ana akili kama sungura, anakoroga kimombo kuliko hata waziri mwenyewe hapa hahahaaaa.
” Acha maneno yako wewe mwarabu, mimi bwana nimekuja hapa kwa mambo mawili, tusiongee saaaaana kupoteza muda. Alisema akimkatisha.
” Naam!
” Laa kwanza kukusalimia.
” Nashukuru sana, kiukweli nashukuru.
” Hilo ndio la kwanza na La pili bhana, sisi ndio wazee tuliobakia katika serikali yetu hii ya Zanzibar.
” Ndio, kweli, kweli kabisa. Waziri alimuitikia akitikisa kichwa juu chini chini juu.
” Ninapoona jambo lolote linaenda kinyume na sheria lazima niumie na kabla halijafika mbali lazima nilifikishe kwako ili tujadiliane kwanza.
” kweli kabisa maalim.
” Sasaa!. Alisema akiwa anaingiza mkono mfukoni na kutoa kivideo kidogo kilichokuwemo. Hii nini mheshimiwa!? ,, alimuuliza akiishikilia kwa juu.
” Kama sikosei ni video kamera.
” Umepatia kabisa ila hii si video kamera tu, hii pia ni Audio reccoder huwa inanisaidia sana katika kumrekod mtu bila kujijua, washa kompyuta yako usikie vitu.
Waziri alicheka huku akifunua laptop yake iliyokuwa pembeni na kuiwasha.
Mzee shaibu nae alifungua kamera na kutoa memory, akamwambia achomeke ataona ujumbe wowote wa kurekodiwa leo uusikilize.

Waziri aliichukua memory huku laptop tayari ilishawaka, akachukua kifaa maalum cha kuchomekea memory kisha akaweka katika laptop.
” Umesema rocod ya leo sio! Aliuliza.
” Yeah, muda si mrefu.
” Nadhani Itakuwa hii hapa.
Waziri aliifungua rekod aliyoambiwa akaanza kusikiliza ukimya ukiwa umetanda.

Macho yalimtoka baada ya kusikia sauti ya moja ya watu wa idara yake akizungumzia jinsi alivyokula rushwa mpaka kuuza matokeo ya kijana aliekuwa anamsomesha green school kwa pesa zake kutokana na upeo wa akili alizokuwa akizionesha.
Aliusikiliza mpaka mwisho, alipomaliza aliachia pumzi kubwa akaegamia kwenye kiti chake akiwa amechoka.
” Nadhani umesikia mambo hayo. mzee shaibu alimuuliza waziri baada ya kuona tayari amemaliza.
” kiukweli kwanza kabisa nashkuru sana hili jambo kulifikisha kwangu kabla ya kwengine maana ingekuwa aibu, na hapo ndio naona umuhimu wa uzee na busara zake, mpigie Cm kwanza Seid ikiwezekana aje hapa nimpe pole.
” Usijali, yuko hapo tu nje na huyo kichwa wako. Alisema. Alitoa cm lock iliyokuwa mkononi na kumpigia mwanae ili aje na mwenzake kwenye ofisi ya waziri.
Hazikupita dk tatu tayari seid na hamad waliingia ndani, Hamad alipofika alimuangalia waziri na kuachia tabasam, waziri nae huzuni aliyokuwa ameipata gafla aliiweka pembeni akaachia kicheko, walikuwa marafiki wa karibu sana, na urafiki wao ulisababishwa na hamad mwenyewe kupenda kuweka ukaribu sana na watu muhimu hasa anaohisi watamsaidia kimasomo.
” Kama wakipatikana viongozi kumi katika serikali yetu wakawa kama wewe waziri, basi hakika Tanzania yetu inaendelea..
Hamad aliongea akisogea alipo waziri, waziri aliinuka akampa mkono akambusu na kumkaribisha seid, aliachia kicheko chengine akiwa anarudi kukaa kwenye kiti chake huku akiuliza.
” kwa nini unasema hivyo kijana.

” Kwa sababu wewe ni waziri ambae umepita uwaziri, huna mambo ya viongozi wa kiswahili, unautendea kazi usomi wako, lakini kuna viongozi wengine wakikaa kwenye kiti cha kazi, wao wanawaza wazile vipi mali za umma na sio kazi. Alisema Hamad.
Waziri alifurahi sana kutokana na kijana hamad anavyoongea.
” Basi inatosha, ukianza maneno yako kijana hatutoongea chochote hapa. Alisema waziri akaomba waendelee na mambo mengine, alirudi kwenye point ya msingi na kumpa pole Seid, alichukia sana kwa tendo lililotendwa juu ya kijana huyo bila yeye mwenyewe kujua.

” Siwezi kufanya kazi na mtu ambaye ni mla rushwa, Nitaitaji ajiuzuru wakati wowote ule na sehemu yake aingie mtu anaeitaji kazi kama yake. waziri alisema kwa sauti ya juu kidogo.
” Mimi hapo nakuunga mkono waziri wangu, but till now i don’t about teacher, dad tell us about him please. ( ila mpaka sasa sijui kuhusu mwalimu, baba tuambie kuhusu yeye tafadhali), nilikuuliza juu juu kwa sababu nilikuwa na presha, bila shaka utakuwa umeenda hospitalini tuambie anaendeleaje na nani ameiba haya matokeo tumjue.

Hamad aliuliza akionekana kuwa na uchungu, mzee shaib ilibidi afunguke kila kitu, namna Zubeir alivyotia mkono mrefu wa pesa kisha kutoeka, jambo ambalo hata waziri mwenyewe alijua hiyo kesi kama kuna mkono wa zubeir ishaisha, kwani ni mtu ambaye anaidai mpaka serikali kwa pesa alizonazo.
” Yani yule mtoto wake kumbe kafeli mpuuzi mkubwa. Hamad alidakia.
” Hivi rafiki yangu, Yule jamaa kila akija darasani ana ipad, samsung sijui malaptop afaulu kweli? Seid aliongea akiwa anamuangalia Hamad.

” Rafiki yangu mimi nilikuambia itajulikana tu na kuna mkono wa mtu mrefu hapa, si unaona, mr richard kaenda dar, kama kuna mkono wa huyu jamaa, anaenda kuendelea kula bata huko baada ya kutumikia jela, kwa namna hii mi sisomi eti niitumikie Tanzania, bora nikose uzalendo kuliko kulitumikia linchi la kipumbavu namna hii. Alisema hamad kwa uchungu.
” Nashukuru sana mheshiwa waziri na mzee wangu hapa kwa kuonesha moyo wa kufatilia matokeo yangu, kiukweli sitoweza kuwalipa mpaka naingia kaburini zaid ya kuwaombea dua tu. Seid alisema baada ya hamad kumaliza kuongea.

Waliongea zaid ya nusu saa mbele, mawasiliano katika vyombo vya habari yalipelekwa haraka ili kutangaza utoaji mpya wa matokeo kutokana na matatizo yaliyotokea, huku profesa sharif akiambiwa ajiuzulu kabla sheria haijachukua mkondo wake na kuumbuka.
Walitoka kwa waziri, Mzee shaibu alirudi nyumbani pamoja na kijana wake, Usiku kidogo ulishaingia, Hamad alimuomba rafiki yake aende na gari lake tu ili asipate usumbufu wa kupanda dala dala kwani tayari yeye ashafika.
” My friend nadhani usiku ushaingia sasa hivi, kwa kuwa unajua kuendesha, chukua funguo hii nenda na gari langu kesho utakuja nalo ukija kuangalia matokeo ambayo kama waziri alivyosema yatabandikwa upya.
” Sawa rafiki yangu, kiukweli wewe ni zaidi ya rafiki kwangu.
” Usijali, nenda mimi nyumbani ni hapo tu.

Seid kwa mara ya kwanza katika maisha yake yote analikabidhiwa funguo za gari ajiachie, mara ya mwisho kupata bahati ya kuendesha ni alipokuwa akijifunza. Aliingia kwenye gari kwa furaha, gari ilikuwa na screen tv ndani aliwasha na kutia midundo, alimchungulia rafiki yake na kumpungia mkono huku akitabasam, meno ya mbele yote yalikuwa nje nje kwa furaha za kuendesha gari kwa mara ya kwanza akiwa mwenyewe.

Maisha yake yote japo kuwa ya tabu lakini alikuwa anapenda sana maisha mazuri, alikuwa anaona yeye umasikini ameupata kwa bahati mbaya tu ila hadhi yake ni hadhi ya watu wenye pesa.
Alikata kona ya round ya bauti ya mjini kuelekea bububu huku akitingisha kichwa na kuchezesha mwili wake kwa ngoma zilizokuwa zinapiga ndani ya gari, Foleni kidogo haikuwepo muda huo hivyo kumpa nafasi ya kubinya mafuta anavyota yeye, huku taswira ya raha moyoni ikimujia na kujikuta anatabasam peke yake.

Mzunguko wa kutangazwa habari za kurudiwa kwa matokeo ya kidato cha sita ndani ya muda mfupi ziliwashtua wengi, maradio mengi yalitangaza habari hiyo, huku Tv ya Z B C nayo ikitangaza habari za matokeo hayo katika kipindi chake cha taarifa ya habari na kupata fununu za chini kwa chini za waziri wa elimu kupiga cm kwa kijakazi wake na kuitaji ajiuzulu kazi ndani ya masaa 24 bila kujulikana chanzo chake nini.

Tukutane Sehemu ya 12

NAMBA YA MWANDISHI 0712384224.

Comments are closed.