The House of Favourite Newspapers

A-Z Mchungaji Msigwa alivyotaka kuzichapa na DC

0

vlcsnap-134012   Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa (mwenye koti katikati) akizozana na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela (wa kwanza kutoka kulia).

Stori: Mwandishi, Wetu Wikienda
IRINGA: Neno zuri linaloweza kutumika ni chupuchupu! Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa nusura azichape na mkuu wake wa wilaya ‘DC’, Richard Kasesela kufuatia mchungaji huyo kupandwa na hasira akidai anahujumiwa.

Ishu hiyo ilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nduli wilayani Iringa ambapo wawili hao na viongozi wengine walikabidhi mabati kwa watu ambao mapaa ya nyumba zao yaliezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.

vlcsnap-133697

Viongozi wengine wakiongea nao baada ya mzozo huo.

Ishu ilianza pale Msigwa alipoonesha kukasirishwa kwa DC huyo kutaka kumuengua kwenye picha ya kukabidhi mabati hayo.Mchungaji Msigwa alimjia juu DC akisema amekuwa akimhujumu kwa siri ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake.

Hali ikawa hivi:
Msigwa: Ananikosea sana huyu, niweke ndani, kaniweke ndani sasa!
DC: Sina shida ya kukuweka ndani.

Msigwa: Sasa! Unadhani nakuogopa! Kuwa na nidhamu, umenikuta hapa, mi nina hasira. Kila siku hata kwenye vikao vyake ananisema! Mi sijalipuka tu.
Msigwa: Unataka kupata umaarufu kupitia mgongo wangu! We kila saa unanisemasema kwa nini bwana? Leo nakutolea uvivu…

vlcsnap-134081

Msigwa anazidi kupandisha ‘Mori’.

DC: Unanitolea uvivu eh, nitolee basi!
Msigwa: (huku akianza kuvua koti) eh! Si kama hivi nakwambia, acha kutafuta ‘cheap popularity’, siasa haiko hivyo bwana! ‘You are using my name? Why are you using my name?’

DC: Sina shida ya kutumia jina lako.
Msigwa: Kila kwenye kikao cha CCM unanisema bwana, acha mambo yako ya kishambashamba, ah! We unadhani mi naogopa kuwekwa ndani?
DC: Sikuitii polisi, sikuweki ndani.

Msigwa: Na sasa hivi nitapambana na wewe serious, sababu unataka kunitania.
Hata hivyo, baadhi ya watu waliofuatilia malumbano hayo kupitia video iliyosambaa mitandaoni, walisema maneno yaliyokuwa yakitoka kwenye kinywa cha Msigwa hayalingani na cheo chake cha uchungaji.

“Kinachoonekana Msigwa ana mengi ya kumhusu DC. Lakini kwa mtu kama mchungaji hakutakiwa kusema haya. Anaposema yeye ana hasira anamaanisha nini? Mchunghaji unakuwa na hasira mpaka unakiri? Ni tatizo,” alisema Hussein Bulagonza, mkazi wa Kijiweni, Iringa.

Walioshuhudia sakata hilo, walimlaumu Msigwa kwa kufyatuka badala ya kutumia vikao halali kama kweli alikuwa na kisasi na mkuu wake wa wilaya.

“Undani wa Msingwa kutaka kupigana na DC ni hasira zake kutokana na mlolongo wa mambo tangu zamani, lakini kwa nini akawa anavuka mipaka ya nidhamu?” alihoji mtu mwingine akikataa kutaja jina lake.

Mtu mwingine alisema Msigwa amekuwa akitafuta nafasi ya kumpasulia DC kwamba, amekuwa akimwandama kwa hiyo siku hiyo ikawa ndiyo nafasi ya pekee kwake.

Leave A Reply