The House of Favourite Newspapers

Abiria Dar Walia Kukosekana kwa Usafiri Ubungo Msimu wa Sikukuu

Taswira ya eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam ilivyoonekana siku ya leo.
Abiria wakisubiri kupanda  daladala ya Mbagara Rangi 3, Simu 2000 (Mawasiliano) iliyopewa kibari cha kusafirisha abiria kwenda mikoani.
Abiria wakitafakari juu ya safari yao.
Abiria wakisubiri kupanda daladala ya Tabata-Kimanga hadi  Simu 2000 (Mawasiliano) iliyopewa kibari cha kusafirisha abiria kwenda mikoani eneo la kituo cha mabasi Ubungo.

 

LICHA ya kuongezwa kwa mabasi yaliyokuwa  yakitoa huduma zake ndani ya Jiji la Dar es Salaam  yaliyopewa vibali vya muda kutoa huduma za kusafirisha abiria kwenda mikoani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, abiria wamekuja juu na kusema mabasi hayo hayakidhi mahitaji yao.

Abiria hao wameyazungumza hayo leo Jumamosi Desemba 23, 2017 katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo Dar, hali inayopelekea baadhi ya abiria kushinda kituoni hapo asubuhi hadi jioni.

Wakizungumza na mtandao huu uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kujionea hali halisi ya usafiri wa mabasi, abiria hao wamesema kama ilivyo kwa misimu mingine ya sikukuu kwa miaka iliyopita msimu huu pia hali ya usafiri ni ngumu kutokana na mabasi mengi kusheheni abiria huku abiria wengine wakishindwa kupata nafasi za kusafiri kutokana na ongezeko kubwa la abiria.

 

Licha ya changamoto ya uchache wa mabasi hayo abiria hao wamelisifia jeshi la polisi kwa namna ambavyo limeimarisha ulinzi na matukio mbalimbali yakiwemo ya kupandishiwa nauli.

 

“Mimi nimekuja hapa Ubungo toka jana, nimelala hapa lakini gari nililokata tiketi bado halijafika hadi muda huu saa sita kutoka Bukoba lakini viongozi wanaohusika na usafirishaji wametupa moyo kuwa muda wowote litaingia, kwani limeshindwa kufika kutokana na kulala njiani,” alisema mmoja wa wasafiri aliyejitambulisha kwa jina la Mayombya.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.