The House of Favourite Newspapers

ACHA ASLAY ATAMBE… ALIFICHWA YAMOTO BAND!

0
Aslay Isihaka.

NAENDA Kusema ndio moja kati ya ngoma ambazo zilimfanya Aslay Isihaka ajulikane kwenye gemu la Bongo Fleva, wakati huo alikuwa chini ya mikono ya Mkubwa Fella kupitia Yamoto Band.

Kadiri miaka ilivyozidi kusogea, imani kwa bwa’mdogo huyo ilizidi kuwa kubwa kwa mashabiki. Walioujua vizuri muziki wake waliweza kumfananisha na wasanii wakubwa tu Bongo lakini swali lao lilikuwa moja, kwa nini hawi juu?

Jibu ni rahisi tu, alifichwa! Sina maana kwamba Mkubwa Fella ni mbaya au alikuwa akimuua kisanii lakini kutokana na mfumo wa kundi, kuna utaratibu ambao lazima muufuate hivyo isingekuwa rahisi kwa Aslay kuachia ngoma kila siku huku wenzake wakiwa kimya.

Aslay ni mwanamuziki na si msanii. Anajua kuimba kwa vyombo, anajua kutunga lakini ingemchukua miaka mia moja kufanya haya anayoyafanya kwa sasa kwa sababu ya utaratibu wa kundi.

Leo hii ametoka kwenye mikono ya Mkubwa Fella, Watanzania wanasikia balaa lake. Hadi naandika makala haya, Aslay yupo namba moja katika ngoma zinazotazamwa zaidi kupitia mtandao ya YouTube.

Ni mafanikio ya ajabu kwani kabla ya kuachia ngoma hiyo, amefanya vurugu kwa kuachia ngoma nyingi harakaharaka kiasi cha kuibua maswali kwamba bwa’mdogo anajiamini nini?

Good news ni kwamba, kila ngoma aliyoitoa, mashabiki wameikariri. Kuanzia Likizo, Mhudumu, Pusha na hata Rudi. Sasa hivi kila kona unayokatiza mtaani, Natamba ndio wimbo wa taifa.

Inapigwa hiyo pamoja na ngoma zake nyingine. Kuonesha kwamba bwa’mdogo huyo upepo ni wake, staa mkubwa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ juzikati alimpongeza na kuonesha anamkubali.

Huu ni wakati wa bwa’mdogo huyu kujipanga vizuri kwani mara nyingi wataalamu wa mambo wanasema muziki hauna mwenyewe. Sasa hivi yupo namba moja, anapaswa kujiwekea mikakati mizuri ili hata baadaye atakaposhuka, awe tayari na miradi mbalimbali ya kumuingizia kipato.

Akibweteka, akilewa sifa, anaweza kujikuta akiangukia pua kama ilivyotokea kwa mastaa wengine ambao kipindi flani walikuwa juu, wakawa na pesa ndefu lakini sasa hivi wameshuka chini kabisa.

Nilisikia anaye meneja, anapaswa kumpima meneja huyo na kuona ana sifa za kumfikisha mbali? Kama anazo basi wajipange vizuri katika kuhakikisha wanaendelea kuwa juu kwa muda mrefu na kujiwekea miradi mingi!

ERICK EVARIST

Leave A Reply