The House of Favourite Newspapers

Rayvanny Atua Airport Na Tuzo 5, Alizoshinda, Ajibu Kuhusu Kumuimbia X- Wake Paula – Video

0

Staa wa Bongofleva, Rayvanny usiku wa kuamkia leo Jumatano, ametua Tanzania akitokea nchini Kenya ambapo alifanikiwa kushinda Tuzo 5 za EAEA (East Africa Arts Entertainment Awards), zilizofanyika nchini humo.

Katika tuzo hizo Rayvanny aliibuka mshindi katika vipengele vifuatavyo;
1. Msanii Bora wa Kiume – East Africa.
2. Album/EP bora – East Africa
3. Mwandishi bora – East Africa
4. Best lovers’ choice single – East Africa
5. Best inspirational single – East Africa

Baadhi ya mastaa wengine wa Bongo walioshinda tuzo hizo ni Diamond Platnumz na Harmonize.

Akizungumza baada ya kutua uwanja wa ndege Rayvanny amesema: “Kwanza namshukuru Mungu kwa mafanikio haya, tuzo nimezoea kushinda lakini kushinda tuzo tano kwa siku moja hii ni mara ya kwanza kwangu.

“Nafurahi kuona tunazidi kupeleka mziki wa Tanzania mbele na ndio maana mnaona sichoki kuzunguka na kufanya kazi na wasanii mbalimbali duniani. Natarajia kutoa wimbo tarehe 26.

“Kuhusiana na wimbo wa hongera nilitunga kwa ajili ya Wanawake wote ambao wanapitia mengi mpaka kutuzaa. Marioo ni familia yangu na nafahamu anatarajia mtoto hivyo ni kwa ajili ya Marioo na Paula pia, sina ugomvi na Paula japo sina mazoea naye kwa sasa kwa kuwa ni mke wa mtu ana familia yake nami nina yangu.”

Leave A Reply