AFCON U17: Serengeti Boys Washinda dhidi ya Angola Bao 2-1

Dakika ya 93: Mwamuzi anamaliza mchezo, Serengeti inapata ushindi wa mabao 2-1.

Dakika ya 92: Makame anaijaribu kuingia na mpira ndani ya eneo la 18 la Angola inashindikana.

Dakika ya 89: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, kasi ya mchezo ni kubwa.

Dakika ya 87: Mchezo unakuwa na kasi kubwa, Serengeti wanashambulia kupitia kwa Mkomola lakini walinzi wanakuwa makini.

Dakika ya 85: Shambulizi kali kutoka upande wa kulia, inapigwa krosi lakini Angola wenyewe wanashindwa kutumia nafasi wanayopata.

Dakika ya 80: Angola wanajipanga na wanatengeneza mashambulizi.

Dakika ya 74: Serengeti wanapata nafasi ya wazi ya kufunga lakini wanashindwa kutumia nafasi, beki wa Angola anaokoa.

Dakika ya 70: Serengeti bado wanaendelea kumiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya Serengeti wanfanya mabadiliko, anatoka Assad Juma anaingia Makame Muksini

Serengeti wanapata bao la pili kupitia kwa Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanya na Mkomola.

Dakika ya 69: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 68: Mchezo unaendelea kwa kasi kwa timu zote kushambuliana lakini wachezaji wa Serengeti wanakosa umakini wakifika mbele ya lango la Angola.

Dakika ya 63: Angola wanafika kwenye lango la Serengeti lakini walinzi wanakuwa makini wanaondoa hatari inayojitokeza.

Dakika ya 58: Mkonola amepata nafasi moja lakini akawa ameotea, amepata nafasi nyingine akaweka mpira wavuni kwa kichwa lakini tayari alikuwa anmeshaotea.

Dakika ya 55: Mkomola wa Serengeti anakuwa msumbufu kwa walinzi wa Angola.

Dakika ya 50: Serengeti wanafika langoni kwa Angola lakini wanashindwa kutumia nafasi wanayopata.

Dakika ya 46: Mchezo umeanza kwa kasi.

Kipindi cha pili kimeanza

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Dakika 45: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza, matokeo ni 1-1.

Dakika ya 41: Angola wanafila langoni mwa Serengeti.

Dakika ya 40: Mchezo sasa ni wa pasi muda mwingi lakini zaidi Serengeti ndiyo wanaomiliki mpira.

Dakika ya 35: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 32: Serengeti Boys wanapata faulo nje ya 18 ya Angola, inapigwa shuti linapaa juu ya lango.

Dakika ya 30: Mchezo unaendelea kasi inaanza kuongezeka.

Dakika ya 22: Serengeti wanajipanga wanashambulia kwa umakini sasa hivi.

Dakika ya 18: Angola wanapata bao la kusawazisha kutokana na mpira wa krosi, walinzi wa Serengeti wakafanya uzembe. Mfungaji wa bao hilo ni Pedro

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 15: Angola wanaanza kuamka na kushambulia.

Dakika ya 10: Mchezo unaendelea lakini Serengeti wanamiliki mpira kwa dakika kadhaa sasa.

Kelvin Naftal anaipatia Serengeti bao kwa njia ya kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa kutoka kulia mwa uwanja.

Dakika ya 6: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!

Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo, timu zote zinasomana.

Mwamuzi anaanzisha mpira.

Zinapigwa nyimbo za taifa na timu zote zimepanga mstari.

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ambacho kipo nchini Gabon kushiriki michuano ya Afrika, kinatarajiwa kushuka uwanjani kucheza dhidi ya Angola, tayari majina yameshajulikana na wachezaji wenyewe ni hawa hapa.

Ramadhan Kabwili
Kibwana Ally
Nickson Kibabage
Dickson Job
Ally Msengi
Enrick Vitalis
Abdul Suleiman
Ally Ng’anzi
Yohana Mkomola
Kelvin Naftal
Assad Juma


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment