The House of Favourite Newspapers

AFDB YAMWAGA BILIONI 630 ZA UJENZI WA BARABARA ZA LAMI MIKOA YA PEMBEZONI MWA NCHI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Patrick Mfugale (kushoto) akibadilishana mikataba na viongozi watakaojenga barabara hizo.
Viongozi hao wakitiliana saini.

 

Benki ya Maendeleo ya Afrika –AFDB imetoa msaada wa shilingi za Kitanzania Bilioni 630.25 kwa serikali ya Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara zilizopo katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.

 

Akipokea msaada huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameishukuru benki hiyo na kumtaka mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuhakikisha anashughulikia vyema utekelezaji wa miradi hiyo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Patrick Mfugale akizungumza katika hafla hiyo alisema:

“Leo Desemba 11, 2017 mikataba minne yenye jumla ya urefu kilomita 402.979 kwa gharama ya shilingi bilioni 562 imesainiwa kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa niaba ya serikali na wakandarasi wanne walioshinda zabuni hizo ambao miongoni mwa makampuni hayo ni Jiangxi Geo-Engineering Group zote za nchini china,” alisema Mbarawa.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele amemshukuru Rais Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kujenga barabara katika Mikoa ya Tabora na Katavi ikiwa ni utekelezaji wa ilani aliyoitoa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Barabara zilizopata ufadhili huo ni pamoja na ile ya Uselula-Komanga –Sikonge yenye urefu wa km 108, Komanga-Kasinde- Inyonga yenye km 108 na barabara ya tatu ni kutoka Kasinde – Mpanda mjini yenye urefu wa km 105.

 

NA DENIS MTIMA/ GPL

Comments are closed.