The House of Favourite Newspapers

African Lyon wana jezi pea moja tu

KWELI hali ni mbaya kwa upande wa kikosi cha African Lyon baada ya nyota wake kuwa na jezi pea moja tu kwa ajili ya mazoezi jambo ambalo linawapa ugumu wakati mwingine.

African Lyon kwa sasa inapitia kipindi kigumu ambacho kimesababisha hata timu yao kukimbiwa na kocha wao pamoja na mchezaji ambaye walimsajili kutoka Ufaransa.

 

Lyon ni kweli wana hali mbaya sio siri unajua kwa sasa wana jezi pea moja pekee kwa mazoezi na mambo yakiendelea hivyo ipo siku tutakuja kuwashuhudia wakifanya mazoezi na nguo zao za kawaida kabisa.

 

“Mmiliki wa timu amekuwa akijitahidi kupambana kuhakikisha anaweza kuiendesha timu na kuona inafika mbali lakini ndiyo hivyo ukata unamsumbua na timu yenyewe haina hata wadhamini hadi sasa,” kilisema chanzo chetu ingawa Rahim Zamunda, kiongozi mkuu wa timu hiyo hakutaka kufafanua chochote.

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Comments are closed.