The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: TIGO FIESTA 2018 YASITISHWA DAR

 

KAMATI ya Maandalizi ya Kilele cha Msimu wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018 imetangaza kusitisha tukio hilo ambalo lilipangwa kufanyika leo Jumamosi, Novemba  24, 2018 katka Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa madai ya sababu zilizo nje ya uwezo wao.

 

Clouds Media Group kupitia kurasa zao za mitandao za CloudsFM na Clouds TV, waandaaji hao wameomba radhi kwa umma kutokana na kilichotokea.

 

Hata hivyo, jana usiku kulikuwa na tetesi kupitia barua ambayo haikuthibitishwa kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilikatisha kibali cha kufanyika Fiesta Leaders Club, Dar es salaam kufuatia ofisi kupokea malalamiko ya wananchi na wagonjwa waliyolazwa hospitalini kutokana na matangazo yaliyoambatana na muziki uliyopigwa kwa sauti kubwa.

 

ITAZAME KWA UPANDE WA VIDEO HAPA

Comments are closed.