‘African Women And Beyond’ Kuwawezesha Wanawake Wa Tanzania
Baadhi ya akina mama waliojiunga na taasisi hiyo pamoja na waanzilishi wa taasisi husika wakishiriki katika uzinduzi huo.Mapaparazi wakichukua matukio katika hafla hiyo.Mwanzilishi wa taasisi hiyo, Joe Kariuki (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taasisi hiyo nchini TanzaniaWaanzilishi wa taasisi hiyo, Maetine Kappel (kushoto) na Joe Kariuki.Mmoja wa akina mama wa Tanzania, Jyot Ajay Ladwa (katikati) akijisajili.
TAASISI ya African Women and Beyond imepanga kuwawezesha wanawake wa Tanzania kwa kuwapatia mikopo nafuu na mafunzo ya biashara ndogondogo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa taasisi hiyo, Joe Kariuki, alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwanzoni mwa mwaka huu nchini Kenya ikiwa na lengo la kuwawezesha akina mama wafanyabiashara ndogondogo na wakubwa kuwainua kiuchumi kwa kuwapa mafunzo na mbinu za kufanya biashara.
Kariuki alisema, wanawake zaidi ya 4,000 nchini Kenya wamefanikiwa kujiunga na taasisi hiyo na tayari wanaendelea kupata mafunzo na elimu juu ya uendeshaji wa mitaji yao.
Aliongeza kwamba sasa Watanzania wanayo nafasi ya kuwezeshwa kujiunga na taasisi hiyo.
“Wananchi hapa nchini ambao watakuwa wamejiunga kwa kujaza fomu maalum wataungana na Wakenya mwezi Machi 2016 kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kufahamiana kwa kujenga uhusiano mwema miongoni mwao,” alisema.
NA DENIS MTIAMA/GPL
Comments are closed.