The House of Favourite Newspapers

Aggrey Morris Kukaa Nje Miezi Miwili

NAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati,q Azam FC, Agrey Moris, anatarajia kuwa nje ya  dimba kwa muda wa miezi miwili ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Misri juzi.

 

Morris aliumia kwenye mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Misri wakati ikijiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea kutimua vumbi nchini humo.

 

Ripoti ya Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyekwenda nchini humo kushugulikia matibabu yake,  inaeleza  beki huyo kisiki alikuwa na uvimbe kwenye kisahani kidogo juu ya goti (patella) na kuchanika kidogo kwa mtulinga wa pembeni wa goti lake.

 

“Aggrey amefanyiwa operesheni kuondoa uvimbe huo na kufanyiwa ‘repair’ kwa mtulinga wa pembeni wa goti lake na ameelekezwa mazoezi ya kufanya kwa wiki mbili, baada ya siku 14 kutoka alipofanyiwa upasuaji atatolewa nyuzi na ataanza mazoezi ya GYM moja kwa moja,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Aliongeza kuwa baada ya siku 21 (wiki tatu) tokea afanyiwe upasuaji, mchezaji huyo mwandamizi wa Azam FC ataanza mazoezi ya kukimbia kidogo-kidogo huku akitarajia kurejea dimbani kwa ajili ya ushindani baada ya siku 60 kupita.

 

Beki huyo  amekuwa nguzo muhimu ya ulinzi tokea kujiunga na Azam FC mwaka 2009 akitokea Mafunzo ya Zanzibar msimu uliopita,  na ameiongoza timu hiyo kutwaa mataji matatu; Kombe la Kagame, Mapinduzi na la Shirikisho la Azam Sports.

 

MAPYA Ya Mama KANUMBA “Baba KANUMBA Alikuwa MCHEPUKO Wangu ” | KATA MBUGA

Comments are closed.