The House of Favourite Newspapers

Ahmed Ally: Bado Nafasi ya Ubingwa Tunayo

0
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwabado wana nafasi ya Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kama watashinda michezo yao miwili inayofata.

“Mechi ya leo tukipata ushindi tutakuwa tumejiweka sehemu nzuri kuelekea mchezo wa tarehe 20/04/2024 dhidi ya mtani wetu. Michezo hii miwili ni lazima tupate ushindi kama tunataka ubingwa.

Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC imeshikwa na michezo hii miwili. Sisi tunawachezaji wenye uwezo wa juu twendeni Wanasimba tukachukue alama sita za michezo hii. Inawezekana sana kama kila mmoja ataingia vitani kuipambania Simba.”

“Imani yangu inaniambia kesho tutapata matokeo mazuri. Lakini njia ya kufikia hii ni Wanasimba kuja uwanjani, Wanasimba kupambana.”

“Hii Simba sio ya mtu mmoja, hii Simba ni ya kila mtu. Jukumu la kuisaidia Simba kupata mafanikio ni la kila Mwanasimba. Wapo watu wanatoka hadharani kutukana viongozi lakini lazima tuwe na mfumo mzuri wa kutoa maoni. Ukiongea hadharani kuna wapinzani unawapa faida sababu hawawapendi viongozi wetu na hawakupendi wewe, wanafurahia sababu tunajivua nguo wenyewe.”

“Kuanzia msimu ujao tumekusudia kufanya mabadiliko kwenye uendeshaji ili tufanye sajili bora. Mtuamini tunaenda kufanyia kazi na hili tayari limeanza kufanyiwa kazi.”

“Uzuri Singida ndio mmetoa mwekezaji wa kwanza wa Simba, @moodewji. Mchakato wa mabadiliko unaelekea ukingoni na mchakato wa kudahili wanachama wapya utaanza hivi punde. Mtatangaziwa Wanasimba wote mnaotaka kujisajili kuwa wanachama ili mfanye hivyo.”- Ahmed Ally akiongea na Wanasimba wa Singida.

Leave A Reply