The House of Favourite Newspapers

Aina 3 za Sickle Cell Unazopaswa Kuzijua

0

Tabibu wa Uwazi | Afya

KUNA aina tatu za upungufu wa damu mwilini kitaalam huitwa sickle cell na kila mtu anapaswa kujua hilo.

Watu wengi wanapoelezwa na wataalam kuwa wana ugonjwa wa sickle cell huwa hawajali kutaka kujua ni aina gani ya ugonjwa huo unaowakabili.

Ni vema wasomaji wa safu hii wakajua kuwa ugonjwa huu upo wa aina tatu na wanapopimwa daktari awabainishie kuwa ama wana ule uitwao kitaalam sickle cell anemia (ss), au unaojulikana kama sickle beta plus ama sickle hemoglobin (sc) na magonjwa yote hayo hugundulika kwa vipimo.

VIPIMO

Ili mtu ajue kama ana ugonjwa huo au la, atalazimika kwenda hospitali na kupimwa na wataalam ambao watatumia kipimo kiitwacho hemoglobin eloctrophonesis. Mtu yeyote akipimwa kwa kutumia kipimo hicho atajua aina ya hemoglobin aliyonayo. Kwa baadhi ya watu wana ugonjwa, lakini hawajitokezi, kitaalam huitwa sickle cell trait.

Hawa ni wale watu ambao wamerithi (heritage) damu ambayo hemoglobin zote A na S huzalishwa katika chembechembe nyekundu za damu (red cell) lakini zile aina ya A huwa nyingi ukilinganisha na zile za S.

Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba wale wote wenye sickle cell trait huwa wana afya nzuri kama watu wasio na tatizo lolote la kiafya.

SICKLE CELL HUAMBUKIZA?

Kuna baadhi ya watu hupenda kuuliza kama mtu kuwa na ukosefu wa damu mara kwa mara kunasababishwa na maambukizi, ukweli ni kwamba ugonjwa huu hauambukizi bali ni urithi na kurithi.

Mtu anarithi ugonjwa huu kutoka kwa wazazi wake kama ambavyo baadhi ya watoto aina ya damu, rangi ya ngozi au nywele n.k ama kurithi hemoglobin kutoka kwa mama au baba yake mzazi.

MATATIZO KWA MGONJWA WA SICKLE CELL

Mtu anapokuwa na ugonjwa huu damu yake hupungua sana na kushindwa kusafiri katika mirija midogo ya damu mwilini mwake.

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply