The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa Yabadilisha Maisha ya Kijana Mfuga Kuku‏

0

PICT 1

Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) wakipima uzito wa kuku wa kienyeji wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia), anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.  

PICT 3

Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa kati) wakitazama maandalizi ya utunzaji wa kuku wa kienyeji wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia) , anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.

PICT 4Kijana Mohamed Kigumi anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam akiwaelekeza meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kati) na  afisa Uhusiano wa Airtel, jinsi anavyoendesha ufugaji wake wa kuku baada ya kumtembelea nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.

Vijana wengi wana ndoto za kujiletea maendeleo lakini wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu sahihi na kutokuwa na mitaji ambayo ingewawezesha kujiunga kwenye miradi ya ujasiriamali.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeiona changamoto hiyo na kuamua kuwafikia vijana mbali mbali hapa nchini akiwemo kijana Mohamed Kigumi ambaye mpaka sasa ameonesha jitihada za kujikwamua na umaskini kwa kuwawezesha kupata mitaji ama vifaa vitakavyotimiza ndoto zao.

Akiongea katika kijiji cha kiluvya, Muhamed Kigumi ambaye anajishuhulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji, amesema licha ya kuanza kazi hiyo kwa muda mrefu lakini sasa ameanza kuona mafanikio makubwa katika kazi yake kutokana na kujengewa mabanda ya kisasa ya kufugia kuku wake na mfuko wa Airtel FURSA tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akifugia kukuwake kwenye mazingira magumu.

Amesema mabanda ya kisasa aliyojengewa na mfuko wa Airtel FURSA pamoja na kupatiwa msaada wa kuku, maisha yake yamebadilika kwani sasa ameamua kujiajiri katika kazi hiyo  na kumuwezesha kusaidia familia na kuuomba mfuko huo kendelea kuwasaidia vijana wengine hapa nchini.

Akiongea katika mabanda ya kuku ya kijana huyo alipomtembelea hapo jana, meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema kuwa mpango wao wa Airtel FURSA umefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo wamemtembelea   bila kumpa taarifa lakini wamebaini kuwa msaada waliompatia kijana Mohamed umeweza kuyabadilisha maisha yake kutokana na kuwa makini na kazi yake.

Mmbando aliongeza kwa kusema, mpango wa kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 uitwao Airtel FURSA  umeanzishwa na mtandao wa simu za mikononi wa Airtel ili kuwasaidia vijana wa Tanzania wenye ndoto zao ili kuweza kuzitimiza ndoto zao kwa kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kufanyia kazi.

Leave A Reply