The House of Favourite Newspapers

Airtel kubuni Zaidi Kupitia Huduma za Kifedha Nchini

1

Airtel (3)

Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money akielezea huduma ya kisasa ya Airtel Money Tap tap kupitia kadi ya kugusisha na kulipa kwa Airtel Money nchini. Kadi hiyo ya Tap tap kupitia Airtel Money imeungwanishwa moja kwa moja na akaunti ya mteja na anaweza kutumika kulipia chochote hata kama simu imezima kwa usalama kabisa.

· Wateja wa Airtel Money wahakikishiwa huduma bora na zenye gharama nafuu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetangaza kuendelea kuboresha huduma za kifedha na kutoa huduma za kibunifu , zenye gharama nafuu kwa wateja wake zitakazochochea kukua kwa huduma za kifedha nchini

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha huduma za Airtel Money, Aijaz Khan kwa kusema” tunayo mikakati kabambe ya kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Money nchi nzima. Tunayofuraha kuwa mstari wa mbele katika kuleta huduma za gharama nafuu nchini. Mwanzoni mwa mwaka Jana Airtel tuliingia katika makubaliano ya kwanza nchini na Afrika na kuwakaribisha makampuni ya simu za Tigo na Zantel ili kuwawezesha wateja kutuma na kupokea pesa mitandao kwa mengine ya simu kwa urahisi zaidi yaani moja kwa moja katika akaunti zao. Leo tunaona fahari kuona tunaogeza wigo huu kwa kuijumuisha kampuni ya simu ya Vodacom kupitia huduma yao ya M-pesa. Tunaamini ushirika huu na makampuni haya ya simu za mkononi kutaleta tija na faida kubwa kwa wateja wetu na kuboresha huduma za kifedha nchini.:

“Tukiwa kama kampuni inayokuwa kwa kasi kwa idadi ya watumiaji na ubora katika kutoa huduma za kifedhai ya airtel , pia tumebuni huduma nyingine ndani ya Airtel Money ambazo zimechangia katika kubadili maisha ya watanzania wengi. Huduma hizi za kibunifu zikiwemo za mikopo ya haraka na isiyokuwa na dhamara kwa wateja na mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama Timiza ambayo hadi sasa imeweza kutoa kiasi cha mikopo yenye dhamani ya zaidi ya shilingi bilioni 90. Vile vile uwepo wa Huduma ya malipo kwa kupitia kadi ya Airtel TaTap imeendelea kurahisisha na kuleta njia mbadala ya kufanya malipo kwa usalama zaidi” alieleza Khan

Aliendelea kwa kusema “ kupitia ofa yetu kabambe ya “Airtel Money Okoa Mapene” tumeendelea kuwahakikishia wateja wetu huduma zenye gharama nafuu kwani kutuma pesa ni bure kabisa

Huduma ya Airtel Money pia imetoa ajira kwa mawakala zaidi ya 15,000 waliondikishwa nchi nzima, huduma hii inapatikana kwa kupiga *150*60# na kuingia kwenye orodha ya Airtel Money na kufanya miamala unayohitaji ikiwemo, kufanya malipo, kuweka na kutoa pesa, kuunganisha na watoa huduma mbalimbali na kufanya malipo ya bidhaa na huduma kwa njia rahisi na salama zaidi ikiwemo kulipia DAWASCO, ZUKU, DSTV, Ada za shule pamoja na visa za US na Zaidi sana mteja wa Airtel ataweza kutuma pesa kwenda Tigo, Zantel na Vodacom na pesa hiyo ikaingia moja kwa moja kwenye akanti zao.

1 Comment
  1. RUKAIYA says

    NAWAPONGEZA KWA HATUA MLIYOFIKIA NA HUDUMA ILIYOTUKUKA KWA KUTURAHISISHIA WATEJA

Leave A Reply