The House of Favourite Newspapers

Airtel Yatangaza mshindi wa milioni 50 wa promosheni ya Jiongeze na Mshiko

0

picha 1
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akiongea na mshindi wa droo ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”, Sylvester Kucas Boyo, mwanafunzi na mkazi wa Shinyanga alijishindia mil. 50 na Juma Sekele Maruka, Mwalimu mkazi wa Nyakato, Mwanza wateja wawili wa Airtel waliibuka washindi, (kushoto) ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya KJubahatisha, Humudi Abdul Hussein na Ofisa huduma za ziada Airtel, Fabian Felician, (kulia) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam,

picha 2Ofisa huduma za ziada Airtel, Fabian Felician akichezesha droo kubwa na ya mwisho ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko” ambapo, Sylvester Kucas Boyo na Juma Sekele Maruka waliibuka washindi. Wakishuhudia ni Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) na mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein (kushoto).

Dar es Salaam, Jumanne Novemba 10, 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewatangaza washindi wa droo kubwa na ya mwisho ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”

Airtel imekuwa ikiendesha promosheni ya “Jiongeze na Mshiko” kwa muda wa siku 120 zilizopita na kuwazawadia wateja wake wa kila wiki wa milioni 1 kwa ngazi ya Free/BURE na shilingi milioni 3 kwa wateja wa ngazi ya premium kwa gharama ushiriki wa Tshs300 tu kwa siku.

Leo “Jiongeze na Mshiko” imemzawadia Sylvester Kucas Boyo, mwanafunzi na mkazi wa Shinyanga , shilling milioni 50 baada ya kuibuka mshindi wa droo kubwa ya mwisho wa promosheni hii.

Akizungumza wakati wa droo hiyo ya mwisho, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema, “leo tumefikia tamatati ya promosheni yetu ya “Jiongeze na Mshiko” ambapo mpaka sasa imezawadia wateja wetu zaidi ya shilingi milioni mia moja nchi nzima. Promosheni hii imeweza kubadilisha maisha ya wateja wetu kwa kuwazawadia pesa taslim kila wiki.

“Napenda kuwashukuru sana wateja wetu wote walioweza kushiriki katika promosheni hii ya “Jiongeze na Mshiko” tangu ilipozinduliwa mwezi Julai mwaka huu. Tunaahidi kwamba Airtel itaendelea kuwajali, kuwawezesha na kuwazawadia wateja wetu kila siku. Tutaendelea kuhakikisha tunafungua milango zaidi ya bahati kwa wateja wapya na waliokuwepo, “alisema Mmbando

Promosheni ya Jiongeze na Mshiko inaonyesha dhamira ya Airtel katika kujali wateja wake na kuwawezesha watanzania kutimiza ndoto zao, aliongeza Mmbando.

Airtel pia imemzawadia Juma Sekele Maruka, Mwalimu mkazi wa Nyakato Mwanza shilingi milioni mbili ambaye aliibuka mshindi wa mwisho wa ngazi ya Free wa promosheni hii.

Leave A Reply