The House of Favourite Newspapers

Kwanini Infinix S5 Ni Simu Sahihi Kwako?

0

 

Kila mmoja anapenda kuwa na simu kali na ya kijanja. Kwa kutambua hilo tunakuletea Infinix S5, simu yenye ubora wa karne ya 21, ambayo imeingia sokonI rasmi Oktoba 2019. Kuifahamu zaidi, ambatana na mimi tukiichambua simu hii:

 

Muundo wake

Infinix S5 imekuja na teknolojia ya kisasa kwenye kioo ambapo kamera yake ipo pembeni (hole-punch diplay) na hivyo kukifanya kioo cha simu kuonekana kwa ukubwa wake, tofauti na matoleo ya simu yaliyopita. Kioo cha simu kina ukubwa wa inchi 6.6 (uwiano wa 20:9), ambapo sasa utaweza kujinafasi zaidi unapoitumia.

 

Umbo la simu hii ni la plastiki na linapatikana katika rangi mbalimbali (Quetzal Cyan, Violent na Nebula Black). Ina sensa ya alama za vidole kwa nyuma ambayo inashikika kwa urahisi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taarifa zako.

Upande wa kushoto wa simu kuna sehemu mbili za kuweka laini (Nano-SIM cards), na sehemu ya kuweka memory vard (microSD) ya ukubwa hadi 256GB.

 

Vitufe vya kuongeza na kupunguza sauti vipo upande mwingine. Upande wa chini wa simu kuna tundu la spika (ear/headphones) na sehemu ya kuchomeka USB na chaja.

Boksi la simu linakuja na ‘cover’ la simu, ‘screen protector’ USB cable, kipini cha kutolea laini na chaja.

 

Muundo wa Ndani

S5ina RAM 4GB ukubwa wa kuhifadhi taarifa 64GB. Mambo mengine ni pamoja na Bluetooth 5, dual-band Wi-Fi, Rediao, USB-OTG na GPS. Mfumo endeshi (OS) wa simu hii ni Android 9 Pie na unaboresheka zaidi kwenda matoleo mengine.

 

Mbali na kuwa na Play Store, sehemu ya kupakua programu mbalimbali kama simu nyingine zilivyonayo, S5 imejumuisha pia Palm Store na AHA Games, ambapo unaweza kupakua programu na michezo mbalimbali.

 

Ukiwa unacheza game unaweza kuiweka simu yako kuzuia simu jumbe zisiingie au mtu asikupigie (DnD) ili kutokukusumbua, lakini unaweza kuziacha kama itakavyokupendeza wewe. Eneo la kitufe cha nyumbani (home button) unaweza kuweka muundo unaoutaka wewe kwani kuna chaguzi mbalimbali.

Katika simu hii kuna kitu kinaitwa ‘Intelligent voice broadcast’ ambacho kinakutajia jina la programu iliyoleta taarifa kwenye simu yako, au jina la mtu anayekupigia simu.

 

Uwezo wake na Uimara wa Betri

Simu hii ina uzito wa gramu 178, ikimaanisha unaweza kuitumia kwa mkono mmoja bila kuchoka, na pia wembamba wake ni milimita 7.9.

Utendaji wake ni bora na inaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja bila kupata moto, kukwama au kuzima. Spika za simu zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na hivyo kukufanya ufurahie unapozitumia kusikiliza muziki.

 

Sensa ya alama ya vidole inafanya kazi kwa haraka zaidi kufungua simu, lakini mbali na hilo, simu hii inaweza kutambua sura yako, hivyo ukaitumia kama njia ya kufungulia simu (face recognition).

Betri yake (4000mAh) hitoki, inaweza kutumika kwa saa 13 na dakika 24 mfululizo bila kuchajiwa, lakini matumizi ya kawaida ina uweza wa kukaa hadi saa 36.

 

Kamera

Infinix S5 ina jumla ya kamera tano, ambapo kamera nne zipo nyuma ya simu, na moja ipo mbele.

Kamera kuu ya nyuma ya S5 ina ukubwa wa 16 megapixels (na aperture f/1.8 pamoja na PDAF). Mbali na hiyo kuna kamera yenye 5 megapixels ambayo inatumika kupiga picha za karibu. Pia kuna kamera nyingine yenye 2 megapixels ambayo inatumika kama sense kwa ajili ya picha (portrait mode), na kamera ya nne ni sensa kwa ajili ya mwanga (low light sensor).

 

Mbele ya Infinix S5 kuna kamera kwa ajili ya selfie yenye ukubwa wa megapixels 32, ambayo itakuwezesha kupata picha zenye ubora mkubwa. Hata hivyo unaweza kupunguza ukubwa huo hadi 16 megapixels ili kukuwezesha kupata picha isiyo na ukubwa (MBs nyingi) lakini yenye ubora.

 

Kiwango cha juu cha ubora wa video ni 1080p. Programu ya kamera (camera app) ina mfumo kukuwezesha kupiga picha bora kwa kutumia AI beauty system, ambapo mbali na hiyo kuna mifumo ya AR Stickers na Panorama, yote kwa ajili ya picha.

Leave A Reply