The House of Favourite Newspapers

Airtel yazindua huduma ya wateja kuangalia vipindi vya TV katika simu

0

1Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani), namna watakavyoweza kujiunga na kufaidi habari kupitia huduma hiyo.

2 Mbando (kushoto), akizindua rasmi huduma hiyo kwa kutumia simu yake ya mkononi huku Meneja wa Huduma za Ziada wa kampuni hiyo, Bi Prisca Tembo akishuhudia.

3Mmbando akionyesha namna huduma hiyo inavyopatikana katika simu mara tu baada ya kujiunga.

4Prisca Tembo akifafanua namna ya kujiunga na huduma hiyo.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua huduma ya itakayowawezesha wateja wake kuangalia vipindi vya televisheni mbalimbali katika vituo vya nje na ndani ya nchi kwa kutumia simu zao za mkononi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, kwenye makao makuu ya Airtel eneo la Morocco jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando, alisema kampuni hiyo imelazimika kuanzisha huduma hiyo yenye gharama nafuu ili kuwasaidia wateja wao kupata taarifa mbalimbali popote walipo.

“Airtel TV itawapatia fursa ya kipekee katika kujihabarisha sehemu yoyote watakapokuwa kwa kutumia simu zao za mikononi, kwani huduma hii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kutoa habari kirahisi, mteja wetu ataweza kujiunga kwa bando la siku, wiki au mwezi mzima,” alisema Mmbando.

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

Leave A Reply