The House of Favourite Newspapers

Ajali ya basi yaua watu 45 nchini Afrika Kusini jimbo la Limpopo

0

Watu 45 wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka kutoka kwenye daraja nchini Afrika Kusini.

Basi hilo lililokuwa na namba za usajili za Botswana lilikuwa na jumla ya watu 46 akiwemo dereva.

Basi hilo liliwaka moto baada ya kuanguka takribani mita 50 chini ya daraja.

Kwa mujibu wa timu ya waokoaji Binti mwenye umri wa miaka 8 ndio mtu pekee aliyebaki hai. Miili mingi imeungua moto na haitambuliki huku mingine ikiwa imekwama kwenye mabaki ya basi.

Ajali hiyo imetokea Kaskazini Magharabi katika jimbo la Limpopo.

#EXCLUSIVE: WEMA SEPETU -”SIPENDI MISIBA WALA BABY SHOWER – NAJISIKIA VIBAYA – MOYO WANGU MWEPESI”

Leave A Reply