Ajali ya Lori Morogoro: Wengine 7 Wafariki Muhimbili – Video

MAJERUHI wengine saba wa ajali ya moto waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 15, 2019,  na kufanya idadi waliofariki kwa ajali hiyo tangu siku ya tukio hadi sasa kufikia 89.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha,  amesema mpaka jana saa 5:30 asubuhi, majeruhi 46 waliopelekwa Muhimbili, kati yao wagonjwa 14 walikuwa wamefariki dunia lakini usiku wa kuamkia leo wagonjwa wengine saba wamepoteza maisha na kufanya idadi yao kuwa 21. (Hawa ni wale waliopelekwa Muhimbili pekee).

 

Aligaesha amesema majeruhi wengine 25 wanaendelea na matibabu huku 16 kati yao, hali zao zikiwa siyo nzuri  na wapo katika chumba cha  wagonjwa mahututi (ICU).

 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILI


Loading...

Toa comment