The House of Favourite Newspapers

Ajib aukana mkataba wa Simba SC Sauz

0

Ajib-mpiraIbrahim Ajib

Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
SIKU chache baada ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, sakata la majaribio yake hayo limechukua sura mpya.

Meneja wa mchezaji huyo, Juma Ndambile amesema Ajib alimdanganya wakala wake aliye nchini Afrika Kusini kuwa mkataba wake na Klabu ya Simba umekwisha.

Juma Ndambile ambaye sasa yuko Durban nchini Afrika Kusini akiwa na Ajib, amesema mchezaji huyo, mwanzo hakuwa mkweli.

“Unajua wakala alidhani Ajib amemaliza mkataba na Simba, lakini nikamueleza bado mkataba wake upo. Alimdanganya kwa kweli, hakusema ukweli.

“Lakini tayari nimezungumza na wakala wake, maana asili yake ni Tanzania. Tayari ameelewa kwamba Ajib ana mkataba na Simba,” alisema.

Kwa mujibu wa Ndambile, Ajib alitarajia kuanza majaribio jana katika Klabu ya Golden Arrows inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

“Wakala wake amempa nafasi ya kufanya majaribio katika klabu nyingine ya daraja la kwanza ya Amazulu. Hii itakuwa ni baada ya Arrows kutoa majibu yao au wanaonaje,” alisema Ndambile.

Ajib aliondoka nchini bila ruhusa ya uongozi wa Simba, inaelezwa Ndambile ndiye alimpigia simu Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba mchezaji huyo anaondoka siku inayofuata.

Wakati Ajib akiondoka nchini, huku nyuma, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alinukuliwa akisema kuwa Ajib ni mmoja wa wachezaji walio kwenye mipango yao ya kuwasajili.

Leave A Reply