The House of Favourite Newspapers

Ajibu Apangua Programu za Lwandamina Yanga

KUKOSEKANA kwa nyota kadhaa kwenye kikosi cha Yanga hivi sasa akiwemo Ibrahim Ajibu, imesab­abisha programu za kocha wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina kutoenda vizuri.

Yanga ambayo hivi sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao wa Kombe la FA dhidi ya Reha FC na wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC, inaendelea na mazoezi bila ya nyota wake ambao wapo Kenya kwenye michuano ya Chalenji wakiwa na timu zao za taifa.

Nyota wa Yanga waliopo Kilimanjaro Stars ni Kelvin Yondani, Ramadhan Kabwili, Gadiel Michael, Raphael Daud na Ajibu, huku waliopo Zanzibar Heroes ni Haji Mwinyi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Matheo Anthony.

Mbali na nyota hao kuwa kwenye michuano hiyo, pia Yanga inawakosa nyota wake wengine ambao ni majeruhi kama Thabani Kamusoko. Lwandamina ameliambia Championi Jumatatu: “Japo hivi sasa tunawakosa wachezaji kadhaa ambao wapo na timu zao za taifa na wengine ni majeruhi, lakini tunaendelea hivyohivyo na maandalizi kutokana na mechi zilizo mbele yetu.

“Nadhani watakaporejea wote ndiyo tutakuwa na muda mzuri wa kujiandaa kwa sababu hivi sasa nusu ya wale wanaounda kikosi cha kwanza hawapo, hivyo kuna kitu kinapungua.”

Omary Mdose | Dar es salaam

Comments are closed.