Ajibu, Gadiel wapelekwa Mamelodi Sundowns

WACHEZAJI wapya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Gadiel Michael watakutana na zali la kupelekwa katika Klabu ya Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini ambako timu hiyo inaenda kuweka kambi ya
kujiandaa na msimu ujao.

 

Wachezaji hao watakwenda Mamelodi ikiwa ni eneo ambalo Simba watakwenda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao. Simba watakwenda kuweka kambi eneo la Pretoria ambako wanatokea Mamelodi kisha watamalizia eneo la Cape Town ilipo Klabu ya Ajax Cape Town.

 

Chanzo kutoka klabuni hapo kimeliambia Championi Ijumaa kuwa hadi sasa kila kitu kuhusiana na kambi hiyo kimeenda vizuri ambapo ni suala la timu kwenda tu na kuweka kambi.

 

“Kila kitu kuhusiana na kambi kimeenda vizuri na mambo yote yapo vizuri, kinachosubiriwa ni timu kwenda tu.

“Timu itaanza Pretoria ambapo tutakaa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye kwenda Cape Town ambapo tutamalizia kambi kisha tutarejea nchini kwa ajili ya sasa kusubiri Simba Day na ligi kuu,” kilisema chanzo hicho. Alipotafuatwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema:

 

“Mambo yote ya kambi yapo vizuri, karibuni tu hapa timu itaondoka na kwenda huko kwa ajili ya kambi.”

Loading...

Toa comment