The House of Favourite Newspapers

Akamatwa Akimuuza Mtoto wa Miaka 10 Ili Anunue Pikipiki

0

Jeshi la Polisi nchini Liberia limemkamata na kumfungulia mashtaka mwanaume wa Sierra Leone mwenye umri wa miaka 29 kwa madai ya kujaribu kumuuza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 10 ili kutafuta pesa za kununua pikipiki mpya baada ya aliyokuwa nayo kuibwa.

 

Baada ya kukamatwa, mwanamume huyo aliwaambia maafisa wa uchunguzi katika mji mkuu, Monrovia, kwamba alihitaji karibu $1,000 (£750) kwani pikipiki hiyo, ambayo ilikuwa ya rafiki yake, ilikuwa imeibiwa nyumbani kwake.

 

Aliambiwa njia pekee ya kupata pesa nyingi hivi haraka ni kwenda nchi jirani ya Liberia kujaribu kutafuta mnunuzi wa mtoto wake. Wakati wa mazungumzo mtoto huyo alimfunga na kumfanya kama kuku na sio binadamu ili kuepusha kugunduliwa.

 

Hata hivyo polisi walipokea taarifa, na babake akakamatwa kwani mnunuzi aliripotiwa kuwa njiani kumchukua mvulana huyo kutoka mji nje ya Monrovia.

Leave A Reply