The House of Favourite Newspapers

Akamatwa kwa Kutaka Kumuuza Mwanaye

0

MWANAMKE mmoja nchini Kenya amekamatwa na polisi katika kituo cha Siaya  kwa kosa la kutaka kumuuza mwanaye wa kiume.

 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Sharon Achieng (23)  ametuhumiwa kwa kutaka kumuuza mwanaye aliye na umri miaka mitano katika kijiji cha Anduro, kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Irene, kwa shilingi milioni 2 za Kenya sawa na milioni 45 pesa ya Tanzania.

 

Irene ambaye alipelekewa mtoto huyo ili kumnunua ameeleza kuwa, Sharon Achieng alimleta mtoto huyo huku akisema yeye ni yatima na anaishi kwa bibi yake pia hajawahi kuolewa.

 

Joseph Aloo ambaye ni kiongozi msaidizi wa kituo hicho cha polisi amesema, wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa kujaribu kumuuza mwanaye kwa mtu ambaye anafanya kazi ya ulinzi.

Leave A Reply