The House of Favourite Newspapers

Al Hilal Hawatoboi… Mabosi Yanga Wapiga Kambi Sudan Kuzuia Hujuma

0
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

BAADHI ya mabosi wa Yanga wamepanga kusafiri kuelekea nchini Sudan siku tatu kabla ya mchezo wao wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.

 

Mchezo huo watakaocheza Sudan ni wa marudiano wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa Oktoba 16, mwaka huu.

 

Timu hizo mchezo wa kwanza wataucheza Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe alisema kuwa wamepanga kuwahi kuweka kambi huko kwa ajili ya kuzuia hujuma walizopanga kuzifanya wapinzani wao Al Hilal.

Wachezaji wa timu ya Yanga.

Kamwe alisema kuwa maofisa wa Yanga tayari wapo katika maandalizi ya safari hiyo, na kabla ya mchezo wa hapa nyumbani wao wataelekea Sudan kuweka mikakati ya ushindi ya ugenini.

 

Aliongeza kuwa lengo la kuwahi huko kuandaa hoteli, usafiri, uwanja wa mazoezi na vyakula watakayokula mara baada ya kikosi chao kufika Sudan.

 

“Mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Al Hilal utachezwa Oktoba 16, mwaka huu lakini msafara wa wachezaji wetu, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi wenyewe watafika huko Oktoba 13, mwaka huu.

 

“Lengo la kuwahi huko siku tatu kabla ya mchezo ni kuhakikisha wachezaji wanazoea mazingira pamoja hujuma watakazozitumia Al Hilal.

 

“Lakini kabla ya msafara huo kwenda huko, maofisa wetu wa Yanga wenyewe watasafiri mara baada ya mchezo wetu wa hapa nyumbani,” alisema Kamwe.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

Leave A Reply