The House of Favourite Newspapers

Al Hilal Kesho Hamchomoki kwa Mkapa… Matajiri Yanga Wavamia Kambini

0
Wachezaji wa timu ya yanga wakifanya yao.

KAMATI ya Mashindano ya Yanga, leo Ijumaa usiku imepanga kufanya kikao kizito sambamba na kula chakula cha usiku na wachezaji wake wote wakiwemo Fiston Mayele na Feisal Salum ‘Fei Toto’ kabla ya kesho kuwavaa wapinzani wao Al Hilal ya nchini Sudan inayoongozwa na gwiji wa ukocha Afrika, Frolent Ibenge.

 

Yanga inatarajiwa kuwakaribisha Al Hilal katika mchezo wa hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijijni Dar es Salaam.

 

Kamati hiyo inaongozwa na matajiri tupu baadhi ni mwenyekiti wake Rogers Gumbo, Seif Ahmed ‘Magari’, Davies Mosha na Lucas Mashauri katika kuhakikisha wanapata ushindi nyumbani kabla ya kwenda ugenini.

 

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa lengo la mabosi hao kukutana na mastaa hao ni kuwaongezea morali, motisha kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu kupata ushindi wa mabao mengi kabla ya kwenda kurudiana kwao Sudan.

Bosi huyo alisema kuwa tofauti na kikao hicho, mabosi hao wataangalia mazoezi ya mwisho kambini kwao Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 

Aliongeza kuwa baada ya kuangalia mazoezi hayo, usiku watakula chakula cha pamoja na baadaye kikao kitafanyika ambacho kitawahusisha wachezaji na benchi lote la ufundi.

 

“Kamati ya Mashindano imejiwekea utamaduni wa kukutana na kufanya kikao na wachezaji, viongozi wa benchi la ufundi katika michezo migumu na muhimu siku moja kabla ya pambano.

 

“Hivyo basi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Al Hilal, uongozi umepanga kukutana na wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa ajili ya kuwaongezea hamasa na morali ya kuipambania watakapokuwepo uwanjani.

 

“Kikao hicho kitakwenda sambamba na ahadi ya bonasi kama wakifanikiwa kuwafunga Al Hilal hapa nyumbani na ugenini na kiasi cha fedha kilichopangwa kuweka ni Sh 300Mil, lakini upo uwezekano wa kuongezeka kuzidi hicho,” alisema bosi huyo.

 

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Viongozi wetu walipanga kukutana na wachezaji mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, hiyo ni katika kuwaongezea hamasa na morali. Huo utamaduni tumekuwa tukiufanya katika michezo muhimu. Na mengi yapo yatakayozungumzwa ambayo ni siri ya timu.”

STORI: WILBERT MOLANDI

KOCHA NABI ANAZUNGUMZA MUDA HUU KUELEKEA MECHI DHIDI YA AL HILAL…

Leave A Reply