The House of Favourite Newspapers

Alex Ferguson: Beckham Alibadilika Baada Ya Kuoa Msanii

0
David Beckham akiwa na mke wake Victoria.

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameelezea mabadiliko ya aliyekuwa kiungo wake David Beckham kabla na baada ya kumuoa Victoria ambaye ni msanii wa muziki.

Ferguson anasema: “Hakuwa tatizo hadi alipooa. Alikuwa akiingia kazini na makocha wa akademi wakati wa usiku, alikuwa kijana mzuri sana.

“Kuoa katika eneo hilo la burudani lilikuwa jambo baya – kutoka wakati huo, maisha yake hayakuwa kama mwanzo. Ni mtu mashuhuri sana, soka ni sehemu ndogo tu.”

TAKWIMU ZA BECKHAM UNITED:

Michezo 387

Mabao 85

Asisti 98

Vikombe 10

MATAPELI PAPA wa ARDHI DAR WAANIKWA – WAZIRI SILAA AFUNGUKA – “NATOA MAELEKEZO KUSAIDIA WANANCHI”..

Leave A Reply