The House of Favourite Newspapers

Alfred H. Shauri: Kinara wa Kidato cha Nne Nchini Aeleza Siri yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus (kushoto) akizungumza jambo na wanahabari.

Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne nchini kutoka shule ya Sekondari ya Feza Boys jijini Dar es Salaam, Alfred H. Shauri (katikati) akielelzea siri ya mafanikio yake kwa wanahabari.

Mama mzazi wa Alfred aitwaye Adela Method akimzungumzia mwanaye.

Alfred akimshukuru mkurugenzi wake kwa kumpatia mkono wa pongezi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Feza Boys ya jijini Dar wakimpongeza mwenzao kwa furaha na kumbeba.

       Alfred Shauri akipozi mbele ya kamera.

Mandhari mbalimbali ya shule ya Feza Boys ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Na Denis Mtima/GPL

MWANAFUNZI wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, Alfred H. Shauri, ameeleza siri ya mafaniko yake kuwa ilitokana na kusoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kila alichofanya.

Akizungumza na wanahabari katika Shule ya Sekondari ya Feza Boys alikosoma eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, amesema kitu cha  kwanza katika kila alilofanya ni kumtanguliza Mungu katika masomo yake na cha pili alikuwa sambamba na wazazi wake kuhakikisha anachukua ushauri wao juu ya masomo yake ambapo kwa uapnde wa walimu wake alisema aliwasikilza kwa makini na kuwauliza maswali pale alipokuwa akihitaji msaada na kujisomea vitabu mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus,  alisema kuwa mafaniko ya mwanafunzi huyo yametokana na juhudi zake mwenyewe alizokuwa nazo wakati akiwa shuleni hapo kwani aliweza kuwa wa kwanza pia katika shindano la insha  iliyozikutanisha shule za Afrika Mashariki mwezi Mei mwaka jana.

Video: Mambo Manne Usiyoyajua Kuhusu Mwanafunzi Bora Kitaifa, Alfred Shauri

BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016

BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2016

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.