The House of Favourite Newspapers

Ali Kiba: Serikali iweke mkono Bongo Movie

0

ali kiba

Ali Saleh Kiba (Ali Kiba)

Na Saleh Ally, Lagos
MWANAMUZIKI Ali Saleh Kiba amesema ingekuwa jambo zuri kama wasanii wa Bongo Movie watapewa nguvu zaidi na serikali.
Kiba ameyasema hayo wakati akizungumzia ushindi wa Watanzania Single Mtambalike ‘Rich Rich’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati wa tuzo za African Magic People’s Choice Awards zilizofanyika katika Hoteli ya Eko kwenye Kisiwa cha Victoria jijini Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia jana.
Akizungumza mjini hapa, Kiba alisema kuna mengi yanawezekana lakini lazima kuwe na nguvu ya serikali kama sehemu ya kuunga mkono.
Kiba ambaye alitumbuiza katika tamasha hilo, aliungana na Rich na Lulu kusherehekea ushindi wao wa tuzo hizo kubwa zaidi katika filamu barani Afrika.

Leave A Reply