The House of Favourite Newspapers

Alichokisema RC AYOUB Katika Uzinduzi wa NYANYA CAPTURES! – VIDEO

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mahmoud, amezindua kampuni ya kupiga picha inayoitwa Nyanya Captures…

Kampuni ya Nyanya Captures iliyochukua takribani miaka mitano kutengenezwa hadi kukamilika, ina jumla ya wafanyakazi 20 mpaka sasa ambapo imelenga kuleta mapinduzi ya picha nchini…

Akizungumza na Global TV, RC Ayoub, amesema kwa mara ya kwanza aliletewa wazo la kuanzisha kampuni hiyo na Ofisa Habari wake anayeitwa, Haji Nyanya, na alipolitathimini vizuri akaona lina mantiki ndani yake ndipo alipochukua haraka hatua za kulifanyia kazi.

Moja Kati ya Picha Zilizopigwa na Kampuni ya Nyanya Captures

Aidha RC Ayoub amesema ameanzisha programu ya kuwasapoti vijana mkoani kwake (Youth Empower) ambapo kabla ya kampuni hiyo, tayari ameshawasapoti vijana zaidi ya 200 kwa kuwapa kuku wafuge na kisha wafanye biashara ya kuuza nyama na mayai.

Kwa upande wake, Haji Nyanya, amesema Nyanya Captures itasimama kila mwaka kufanya maonesho ya kimataifa na nusu ya mapato yatakayopatikana yatarudishwa kwa jamii, ambapo ameeleza kuwa kampuni hiyo inayopiga picha na video iko tayari kufanya kazi muda wowote kwenye shughuli yoyote iwe ni harusi, tamasha, kongamano ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara.

Comments are closed.