The House of Favourite Newspapers

Alikiba Apewa Zigo La Mabao Coastal

Alli Salehe ‘Alikiba’

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Alli Salehe ‘Alikiba’ ni kama amepewa zigo la mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kocha wa kikosi hicho, Juma Mgunda kumtaka afunge zaidi ya mabao 25 kwa kile alichodai uwezo wa kufanya hivyo anao.

 

Alikiba tangu asajiliwe na timu hiyo msimu huu, bado hajaoneka­na uwanjani wakati tayari wenzake wameshacheza mechi mbili mpaka sasa na leo Jumamosi wanatarajiwa kupambana na KMC katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa.

 

“Mashabiki wa Coastal Union wa­nachotakiwa kufahamu ni kwamba timu hii imesajili wachezaji 30 na kila mchezaji anataka kucheza, hivyo muda ukifika kila mmoja ataonekana uwanjani.

“Najua wengi wanamuulizia Alikiba, niseme tu ataonekana uwanjani muda si mrefu na niwaambie ni mshambulia­ji mzuri na anaweza kufunga zaidi ya mabao 25 msimu huu,” alisema Mgun­da.

Stori na Adam Mwanyakunga,Tanga

Comments are closed.