Alikiba: Pesa Zinatosha Ndugu Zangu wa Kahama, Acheni Nipafomu Kwanza

Alikiba akiimba jukwaani Kahama mkoani Shinyanga

Staa wa Bongo Fleva, Alikiba usiku wa kuamkia leo amefanya bonge moja la shoo katika Mji wa Kahama mkoani Shinyanga katika sherehe ya kutimiza mwaka mmoja kwa kiwanja maarufu cha burudani katika mji huo cha The Magic 101.

 

Vibe la mashabiki kumtuza staa huyo lilikuwa kubwa kiasi cha mwenyewe kunyoosha mikono na kusema: “Pesa zimetosha ndugu zangu wa Kahama, acheni nipafomu.”

 

Licha ya Alikiba kuwataka mashabiki wasiendelee kumtuza, bado waliendelea kumiminika jukwaani na kumpa fedha pamoja na kupiga naye picha, wakionesha furaha waliyokuwa nayo kwa staa huyo kufanya shoo katika kiwanja hicho cha kipekee na cha kisasa cha burudani katika Mji wa Kahama.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwapigia The Magic 101 kwa namba 0762388130 au 0655000927.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment