The House of Favourite Newspapers

Aliyeandika Kitabu ‘Jinsi Ya Kumuua Mumeo’ Ahukumiwa kwa Kumuua Mumewe

0
Nancy Crampton Brophy (71)

MWANDISHI wa kitabu chenye jina lisemalo ‘Jinsi ya kumuua mume wako’ kutoka nchini Marekani aitwaye Nancy Crampton Brophy, mwenye umri wa miaka 71 amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya mume wake aliyoyatekeleza mwaka 2018.

Nancy Crampton Brophy akiwa na mume wake enzi ya uhai wake

Imeelezwa kwamba tukio la mauaji lilifanyika mahali ambapo mume wake huyo aitwaye Daniel Brophy, alikuwa akifanya kazi kama mpishi na mwili wake ulikutwa sakafuni kwa majeraha ya risasi mbili mnamo Juni 2008.

Nancy Crampton Brophy, alihukumiwa maisha juzi Juni 13, 2022, na kwamba hata silaha aliyoitumia haijulikani ilipo.

Leave A Reply