The House of Favourite Newspapers

Aliyekamatwa na Mabilioni Airtport Aachiwa Huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru na kumrudishia fedha zake, Winfred Busige (33), raia wa Uganda aliyekamatwa akisafirisha fedha kiasi cha TZS bilioni 2, katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKNIA), baada ya kulipa faini ya TZS milioni 100.

 

Winfred ambaye ni Karani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, alifikishwa mahakamani hapo Desemba 22 mwaka jana akikabiliwa na kosa la kushindwa kuelezea kwa mamlaka ya forodha fedha alizokamatwa nazo Airpot ambazo ni USD Milioni moja (zaidi ya Sh.Bil 2).

Wakili wa serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja na kudai kuwa kosa hilo alilitenda kinyume na kanuni za sheria za utakatishaji fedha, ambayo haimnyimi mshtakiwa dhamana.
Businge alidaiwa kutenda kosa hilo December 11, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

BREAKING: CHADEMA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Comments are closed.