The House of Favourite Newspapers

Aliyekataliwa Simba awa kipa bora Ethiopia

ALIYEWAHI kuwa golikipa wa Simba SC, Daniel Agyei amechaguliwa kuwa kipa bora wa ligi kuu nchini Ethiopia.

Agyei aliyeachwa na Simba misimu miwili iliyopita, alisitishiwa mkataba wake wa miaka miwili na Simba kabla ya kutimkia Jimma Abba Jifar FC, mwaka jana.

Mghana huyo aliachwa na Simba kwa kile kilichoelezwa kiwango chake kushuka wakati timu hiyo inafundishwa na Mcameroon, Joseph Omog ambaye naye alitimuliwa baadaye.

Agyei, amechaguliwa kuwa kipa bora timu yake ikiwa imemaliza ligi kwa kuwa mabingwa wa ligi kwa pointi 55 sawa na ST George wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumzia tuzo hiyo aliyoichukua, Agyei aliyetwaa ubingwa wa kwanza akiwa na kikosi hicho, alisema: “Nashukuru kwa kufanikiwa kuchukua tuzo hii ya kwanza kama kipa bora wa ligi, kwani ni moja ya vitu nilivyokuwa nimevipanga.

“Tofauti na tuzo hiyo, pia nashukuru kwa kufanikiwa kuchukua ubingwa huu wa kwanza tangu nimejiunga na timu yangu, hivyo najisikia furaha,” alisema Agyei.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

JESHI USU LA WANYAMAPORI LAZINDILIWA, SERENGETI MARA – VIDEO

Comments are closed.