The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi IFM Amfanyia ‘Sapraizi’ Shigongo

Mwanafunzi wa IFM, Yusuph Abas akimkabidhi Eric Shigongo picha yenye sura yake aliyoichora kwa mkono wake.MWANAFUNZI wa Mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam, Yusuph Abas amemfanyia ‘Sapraizi‘ Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigong baada ya kumkabidhi picha aliyoichora kwa mkono wake.

Mwanafunzi huyo amemkabidhi picha hiyo leo Ijumaa 17, 2018 kwenye Kongamano la Chuo Life Time lililoandaliwa na Taasisi ya Chuo Life Tanzania na kuwakutanisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam wakati Eric Shigongo alipohudhuria kongamano hilo lililolenga kuwatia moyo na namna ya kuishi wawapo chuoni.

Wakati kongamano hilo likiendelea kabla Shigongo hajaanza kuzungumza, ghafla Yusuph alitoka kwenye kiti chake na kupita mbele kisha kusema; “Ninamhitaji Eric Shigongo, nina zawadi yake muhimu siku ya leo,” kisha alifungua mfuko huo na kutoa picha aliyoichora ikiwa na sura ya Shigongo.

Akimkabidhi Shigongo zawadi hiyo, Yusuph amesema nia yake ni kuwatia moyo vijana wengine ili watumie vipaji walivyonavyo kama yeye alivyofanya kwa kuchora picha na kuonyesha appreciation kwa watu ambao wamekuwa wakijitioa kuisaidia jamii na vijana kutimiza ndoto zao.

Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 2016, Dyana ambaye ni mwanafunzi wa IFM naye akiwatia moyo wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Mbali na Shigongo, wengine waliohudhuria na kupata fursa ya kuzungumza na wanafunzi hao ni Mtaalam wa Mambo ya Saikolojia na Mahusiano, Dkt. Chris Mauki, Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward, Benjamin Fernandes na wengine.

Chris Mauki akizungumza na wanafunzi hao.

Akizungumza na wanafunzi hao katika Ukumbi wa Yombo 4, chuoni hapo, Shigongo amewaasa kutokukata tamaa katika kutafuta maisha na kwamba changamoto katika maisha yao ndiyo iwe suluhisho la mafanikio yao kwa kutatua changamoto hizo.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.