Aliyemponza Wema, Madaha Mahaba kama yote

YULE mwanaume aliyemponza msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Patrick Christopher ‘PCK’ baada ya kurusha picha zao za kimahaba mtandaoni na kusababisha Wema apate kesi iliyomsumbua kwa muda mrefu, ameonekana akiwa kwenye mahaba kama yote na mwanadada Baby Joseph Madaha.  PCK na Madaha wameonekana kuwa na mahaba kwa muda mrefu ambapo huko nyuma ilivumishwa sana lakini Madaha alikuwa akikataa kabla ya hivi karibuni kuonekana kwenye picha wakiwa kama mtu na mtu wake live.

Kuonekana kwa picha hizo kulishibisha madai ya wawili hao kuwa wapenzi huku wengine wakifikia hatua ya kusema Baby Madaha amekufa, ameoza kwa jamaa huyo.

“Mnajua Baby na PCK siyo kama wanafanya kiki, ni mapenzi motomoto, wameona isiwe tabu. Watu walisema wee, Madaha akawa anakataa kutoka naye lakini sasa hivi naona ameamua kujiachia,” alisema mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jamila baada ya kuona picha za wawili hao mtandaoni.

Mara ya mwisho Baby na Patrick walionekana kwenye shoo ya Ali Kiba nchini Kenya ambapo walikuwa katika shangwe huku mara kadhaa Madaha akijibebisha.

Kufuatia mahaba hayo, Risasi Mchanganyiko juzi lilifanya jitihada za kumtafuta Madaha ili kujua kama ndiyo kachukua mikoba ya Wema na alipopatikana alisema aachwe na maisha yake kwani anaishi vile ambavyo anajisikia.

Alipobanwa angalau aseme lolote ili kukata kiu ya mashabiki zake ambao wanataka kujua kama PCK ndiye shemeji yao kwa sasa, Madaha alisisitiza kuwa hayuko tayari kuongelea mapenzi, anachojua yeye ni kijana anakula bata na umri unamruhusu.

“Mimi ni kijana bwana, nakula bata mwanzo mwisho hayo mambo ya kuniuliza kuhusiana na mapenzi na Patrick mtajaza wenyewe,” alisema Madaha. PCK hakuweza kupatikana mara kuzungumzia uhusiano wake na msanii huyo.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI MCHANGANYIKO


Loading...

Toa comment