The House of Favourite Newspapers

ALIYEMSAFIRISHA PAKA KWA NJIA YA POSTA YAMKUTA

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Yang (33) nchini Taiwan amepigwa faini ya dola za Taiwan NT$60,000 (sawa na Tsh milioni 4.5) kwa kuvunja sheria ya Ulinzi wa Wanyama ya Taiwan, baada ya kumsafirisha paka wake kama kifurushi kwa njia ya mawasiliano ya posta.

 

Imeripotiwa kuwa Yang alimfungasha paka huyo kwenye kifurushi aina ya ‘Scottish fold’ kwenda kwenye kituo kimoja cha kuhifadhi wanyama nchini humo katika wilaya ya Banciao. Yang amedai kuwa hakuwa na mahitaji tena ya kuendelea kumfuga paka huyo.

 

Kutokana na kosa hilo, alipigwa faini ya ziada ya NT$30,000 kwa kuvunja sheria ya kuzuia na kupambana na magonjwa ya kuambukiza ya wanyamakwa  sababu wafanyakazi wa kituo cha wanyama alipopokelewa paka huyo waligundua kuwa hakupewa chanjo ya kichaa.

Maofisa wa ulinzi wa wanyama wa mjini Taipei walifanikiwa kumnasa mtuma kifurushi hicho kupitia kupitia kamera za CCTV. Mamlaka ya ulinzi wa wanyama inasema paka huyo ana afya njema na baada ya uchunguzi zaidi anaweza kuchukuliwa na mmiliki mpya.

 

Baada ya kunaswa, Yang alijitetea kuwa alijaribu kumgawa paka huyo bila ya mafanikio. Yang pia alidai hakuwa na muda wa kutosha wa kumwangalia mnyama huyo na kumtunza. Paka huyo pia ana matatizo ya kutembea baada ya kujeruhiwa, na licha ya kupatiwa matibabu kadhaa, yakiwemo ya kienyeji lakini bado hali yake haikutengemaa.

 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyama, Chen Yuan-chuan, amelaani vikali mkasa huo akisema: “Mnyama anaweza kupatwa na hali mbaya kwa kukosa hewa ndani ya kifurushi na kupandwa na gadhabu, pia hakukuwa na maji safi na salama.”

 

Yuan-chuan amewataka watu kufuata taratibu halali za kisheria pale wanapoona hawawezi tena kuendelea kuwatunza wanyama wao wa nyumbani.

Comments are closed.