The House of Favourite Newspapers

Aliyeomba kwa Kutumia Kisu Ala Kibano

0

Omba omba (1) Njemba huyo akiwa amekula kibano cha polisi.

Na Francis Godwin, Risasi Jumamosi

IRINGA: Njemba aliyefahamika kwa jina la Mohammed ambaye amekuwa akituhumiwa kuomba pesa mtaani huku wakati mwingine akiwatishia watu kwa kisu pale wanaposita kumsaidia, juzikati alikula kibano cha polisi baada kufungiwa kazi na hatimaye kutiwa mbaroni.

Omba omba (2)Tukio la kukamatwa kwa kijana huyo lilitokea juzikati saa 5 asubuhi, katika eneo la Posta baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hasa wanawake ambapo walipokuwa wakimnyima, amekuwa akiwakimbiza na kisu mkononi.

Mmoja kati ya wanawake ambao waliwahi kutishiwa  kuchomwa  kisu na kijana huyo, Amina Said mkazi wa Mkwawa alisema:

Omba omba (3)“Namekumbana na kijana huyu zaidi ya mara mbili, aliniomba pesa, nilipoonesha kutompatia alinitisha kwa kisu.

“Nikajiuliza ni ombaomba kweli huyu? Unajua Iringa ina ombaomba wengi lakini inapofikia mtu anaomba huku akitishia kujeruhi, ni hatari sana. Yaani anaonekana ni kijana mhuni ambaye ameamua kutumia njia hiyo haramu kujipatia pesa.”

Omba omba (4)Kufuatia kukamatwa kwa kijana huyo, wengi walioongea na gazeti hili walisema kuwa imekuwa afadhali kwani wamekuwa wakitembea wakiwa na hofu kubwa ya kujeruhiwa.

“Bora polisi walivyomfungia kazi, wengi wanamjua kijana yule kwani amekuwa akitumia njia hiyo isiyo halali kupata pesa,” alisema Salum Mikidadi mmoja wa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Posta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba, mbali na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo pia aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wanapoona matukio ya watu kama hao kwani ni hatari katika jamii.

Leave A Reply