The House of Favourite Newspapers

Alidai kuzaa na Mama Diamond ataka DNA

0

mama-diamondMama Diamond.

Stori: MUSA MATEJA NA ISSA  MNALLY, WIKIENDA

Dar es Salaam: Lile sakata la DJ maarufu jijini Dar, Jerry Kato kuibuka na kudai kuwa ndiye baba mzazi wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz, limechukua sura mpya baada ya mwanaume huyo kutaka Vipimo vya Vinasaba (DNA-Deoxyribonucleic Acid) ili kuthibitisha kuwa, mtoto huyo ni wake.

Jerry Kato Jerry Kato.

KABLA YA KUIBUKA MVUTANO
Mapema wiki kadhaa zilizopita, Kato, mkazi wa Boko jijini Dar, aliliambia gazeti pacha la hili, Ijumaa kuwa, kwa muda mrefu jambo hilo limekuwa likiutesa moyo wake kwamba yeye ndiye baba mzazi wa Esma ila anashangaa mama wa mtoto huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ kukwepa kusema ukweli.

ESMA.jpgEsma Platnumz

Katika habari hiyo ambayo Kato alieleza mambo mengi ya namna alivyokutana na mama Diamond wakati akiwa DJ wa Mbowe Club (kwa sasa Billicanas) iliyopo Posta, Dar ambapo alimpa mimba mama huyo ndipo akazaliwa Esma. Katika habari hiyo, mama Diamond alikana kumfahamu Jerry na kwamba alishangazwa na habari hizo hivyo Wikienda likazama mzigoni upya kujua mbivu na mbichi.

JERRY AIBUKA UPYA
Wakati gazeti hili likichimbua, Jerry aliibuka upya na kusema kwamba, naye alishangazwa na kitendo cha mama Diamond kumkana ilihali akijua ukweli wa ishu hiyo. “Nimeshangaa sana kusoma kwenye Ijumaa eti hanijui na kwamba baba wa Esma ni mwanaume aliyemtaja kwa jina la Abdulkadiri ambaye yupo Zanzibar. “Ukweli ni kwamba nimefedheheka na nimeumia sana,” alisema Kato.

ATAKA DNA
Akaongeza: “Kama kweli anaendelea kubisha kuwa, Esma si mwanangu basi namtaka tukapime DNA. Hiyo ndiyo itatoa ukweli wa mtoto ni wa nani? Akubali tu tukapime ili nimchukue mwanangu. “Yaani akikubali tu DNA biashara itakuwa imekwisha maana wala hakutakuwa na sababu ya kulumbana.”

TURUDI KWA MAMA DIAMOND
Baada ya kupata msisitizo wa Kato aliyeonekana kutibuka kwa kitendo cha mama Diamond kumkana kuwa hamjui, Wikienda lilirudi kwa mama Diamond na kumbana tena upya ambapo aliamua kujibu mapigo kwa kufunguka anachokijua.

Mama Diamond: “Unajua mwanzoni nilipoulizwa nilishtuka ndiyo maana nikawa sina majibu ya moja kwa moja kwa sababu sikujua huyo mtu anataka nini?”
Wikienda: “Je, ni kweli kwamba humfahamu kabisa Jerry Kato?”

Mama Diamond: “Jery namfahamu na ni kweli kwamba zamani enzi zetu alikuwa DJ wa Mbowe lakini si kweli kwamba ndiye baba wa Esma kwa sababu baba mwenyewe yupo Zanzibar.”
Wikienda: “Unadhani kwa nini Kato anang’ang’ania kuwa Esma ni mwanaye?” Mama Diamond: “Ni kweli Jerry alikuwa rafiki yetu, tulikuwa tukienda klabu tunakutana naye lakini wakati napata ujauzito wa Esma nilikuwa Zanzibar, hivyo Jerry hahusiki.”

Wikienda: “Yeye anasema hata akiulizwa Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) ambaye wakati huo alikuwa bosi wa Hoteli ya Mbowe atakukumbuka kwa sababu yeye ndiye aliyempa fedha Kato akupe wewe nauli uende nyumbani kwenu Kigoma hadi ujifungue. Je, ni kweli?”

Mama Diamond: “Kwanza akina Mbowe walikuwa na sehemu yao, tulikuwa hatuchanganyikani na wao kwa sababu mimi na wenzangu tuliokuwa tunakwenda klabu tulikuwa wadogo. Si kweli kwamba Mbowe alitoa fedha ili niende kwetu kwa sababu kwanza nilipopata ujauzito nilikuwa Zanzibar.”
Wikienda: “Kato anasema kama unabisha, anataka mkapime DNA ya Esma ili amchukue mwanaye. Je, upo tayari?”

Mama Diamond: “Mimi wala sina neno, nipo tayari lakini je, akikuta mtoto si wa kwake atafanyaje? Je, akikuta ni wa kwake pia atafanyaje?”
Wikienda: “Anasema akikuta ni wa kwake atamchukua au wewe unasemaje?”
Mama Diamond: “Alikuwa wapi mpaka aje kumchukua leo wakati ni mama wa watoto wawili? Kama anataka kupima DNA mwambieni namsubiria.” Juzi, Wikienda lilimtafuta Mbowe kwa njia ya simu lakini hakupatikana.

WIKIENDA BEGA KWA BEGA
Kwa sasa Kato anajipanga kwa ajili ya DNA ya Esma hivyo Wikienda litakuwa bega kwa bega na wahusika hao ili kukujuza majibu.

Leave A Reply