The House of Favourite Newspapers

Ally Hapi Aagiza Polisi Kumweka Ndani Mmiliki wa Kampuni

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani kwa saa 48 mmiliki wa kampuni kuzoa taka ya Total Waste Solution.

Hapi ametoa agizo hilo baada ya Mmiliki huyo kukaidi agizo lake la kuwalipa kwa awamu 3 stahiki zao wafanyakazi wa kampuni hiyo walioachishwa kazi. Jumla ya wafanyakazi 13 wa Kampuni hiyo walilalamika kwa Mkuu wa Wilaya jana kuwa hajalipwa madai yao ya takribani Tsh. Milioni 15.

Aidha, katika kuanza kushughuliki suala hilo jana alimsimamisha kazi Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni, Anord Kinyaiya kwa kushindwa kutatua tatizo hilo.

Comments are closed.