The House of Favourite Newspapers

Ally Sonso: Nakwenda KMC

0

 

ALIYEWAHI kuwa mlinzi wa kushoto wa Yanga, Ally Mtoni Sonso, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kujiunga na KMC kufuatia mazungumzo mazuri ya pande hizo mbili, baada ya kumaliza mkataba wake na Kagera Sugar.

Sonso aliyejiunga na Kagera Sugar kutokea Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita, kwa sasa ni mchezaji huru, na tayari ameanza mazungumzo na baadhi ya klabu zinazomhitaji kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota huyo anatajwa kwenda kuchukua nafasi ya mlinzi wa kushoto wa KMC, David Bryson ambaye tayari amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sonso alisema: “Kwa sasa nimemaliza mkataba wangu na Kagera Sugar, na tayari kuna ofa ambazo zimeletwa mezani kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kusaini mkataba wa kuwatumikia kwa msimu ujao.

“Kuna ofa ya klabu za mikoani, lakini pia kuna ofa za klabu za Dar es Salaam kama vile Ruvu Shooting na KMC, ambazo kutokana na mazungumzo baina yetu naona kuna nafasi kubwa ya kuweza kujiunga nazo.”

STORI:Joel Thomas,Dar es salaam

Leave A Reply