The House of Favourite Newspapers

Alphonce Simbu Awasili Nchini, Akabidhi Medali Yake kwa Mwakyembe (Video)

0
Alphonce Simbu (kushoto) alipowasili Uwanja wa Ndege, Dar.

 

Simbu akionyesha medali yake.

MAMIA ya Watanzania wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wamejitokeza kumpokea Mwanariadha, Alphonce Simbu aliyekuwa akitoka London Uingereza kushiriki mashindano ya kimataifa ya riadha The International Association of Athletics Federations (IAAF).

Simbu aliyeshinda medali ya shaba katika mbio ndefu za Marathon akimaliza nafasi ya tatu katika Mashindano hayo amewsili na wenzake watatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar jioni saa 11 jioni baada ya kuachwa na ndege iliyokuwa awasili saa 6 mchana.

 

VIDEO:  Alphonce Simbu Amkabidhi Medali Waziri Harrison Mwakyembe


Ndugu jamaa na marafiki walijitokeza kuraki Simbu wakiwemo kaka yake, mkewe pamoja na mwanaye ambapo hafla fupi ya kumpokea ilifanyika Uwanjani hapo.

Baada ya kuwasili, simbu aliikabidhi medali yake ya shaba kwa Waziri Dkt. Mwakyembe ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa Wizara yake kwenye tasnia hiyo ya riadha hapa nchini.

Simbu akikabidhi medali yake kwa Waziri Mwakyembe.

 

Simbu alikimbia kwa saa 2:09:51 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Mkenya, Geoffrey Kirui aliyemaliza kwenye nafasi ya kwanza akikimbia kwa saa 2:08:27 na Muethiopia, Tamirat Tola aliyemaliza wa pili akikimbia kwa saa 2:09:49.

Mwakyembe akionyesha medali ya Simbu kwa wanahabri.

 

Ushindi huo wa Simbu ni neema kwa Tanzania ambayo tangu 2005 ilipochukua medali kwenye mbio hizo huko Finland, haijawahi kushinda medali yoyote ya dunia hadi leo Jumapili Simbu kushinda Shaba.

Medali hiyo ya Simbu ilianza kuonekana mapema wakiwa wamekimbia umbali wa kilomita 21 (Nusu Marathon).

Kwa ushindi huo sasa Simbu ataondoka na kitita cha Dola 20,000 huku bingwa akizawadiwa Dola 60,000 na mshindi wa pili ataondoka na Dola 30,000.

 

Leave A Reply