The House of Favourite Newspapers

AMBA LULU: NATAMANI JUX AWE MPENZI WANGU

0

MSANII na mnenguaji kwenye video za wasanii hapa Bongo, Amber Lulu, amefunguka kwamba anampenda mwanamuziki wa Bongo Fleva Juma Jux aka Jux na anatamani awe mpenzi wake.

 

Akizungumza na Global TV Online mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye sherehe ya mwanamitindo Hamisa Mobetto alipokuwa anamfanyia mtoto wake Dylan sherehe, ambaye alizaa na msanii wa Bongo Fleva, Lulu amesema kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake wa sasa (ambaye hakumtaja jina) ila anampenda sana Jux na anatamani awe mpenzi wake, pia alimuomba msamaha Vannessa Mdee kwa kufunguka juu ya mpenzi wake Jux.

 

“Jamani nampenda sana Jux, kabarikiwa sifa zote, ananivutia sana ni mwanaume mwenye vivutio ambavyo mwanamke yeyote lazima apagawe naye, hata akipita mbele ya watu wengi basi kila mwanamke lazima amtizame alivyo mzuri. Pia namuomba radhi Vanessa Mdee kwa haya ninayoyaongea juu ya Jux,” alisema mrembo huyo ambaye aliongeza:

 

“Hata hivyo, mimi nina mpenzi wangu kwa hiyo naye anisamehee tu kwa haya maneno maana na yeye nampenda sana, ila siwezi kumtaja jina kwa sasa ipo siku mtamjua tu mashabiki zangu,” alisema.

 

Amber Lulu ni mwanamke asiyeishiwa skendo kwenye mitandao ya kijamii na kwenye midomo ya watu hapa Bongo, ameweka wazi kuhusu mahusiano yake ya sasa lakini bado hajataja jina la huyo mwanaume wake.

 

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Leave A Reply