The House of Favourite Newspapers

VIGOGO WA CHUO CHA FEDHA WAPATA DHAMANA

0
Watuhumiwa wakipita katika lango la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupata dhamana.
Ndugu wa watuhumiwa wakiwakumbatia kwa furaha baada ya dhamana.

 

VIGOGO wawili wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wanaokabiliwa na kosa la kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 1,097,681,107, wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Vigogo hao ni aliyekuwa Kaimu Mtendaji Mkuu, Shaha Hanzuruni na Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Onesphor Luhungu.

Masharti waliyotimiza ni kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini bondi ya Sh. Milioni 250 ambazo zimetakiwa kupelekwa mahakamani hapo.

Washtakiwa hao pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama ambapo baada ya kutimiza masharti hayo, kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24, mwaka huu.

Watuhumiwa wanakabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kati ya Januari 1, 2012 na Desemba 30, 2014 katika ofisi za TIA zilizopo Temeke wakiwa wafanyakazi wa chuo hicho ambapo hawakufuata taratibu za manunuzi ya kununua ardhi kampasi ya chuo cha TIA Mwanza na kusababisha Vedastus Lukago kupata faida ya Sh. Bilioni 1,097,681,107.

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave A Reply