Amber Lulu afyatuka kutoka na Kusah

HABARI iliyotrendi kwenye mitandao ya kijamii wikiendi iliyopita ni tetesi za msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ kutoka kimapenzi na mzazi mwenza wa msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Rubby’ aitwaye Kusah.

 

Wakati ishu hiyo ikishika kasi mithili ya moto wa kifuu huku zikiambatanishwa picha zao za kimahaba, Amber Lulu amefyatuka anachokijua juu ya ishu hiyo.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Amber Lulu amesema yeye mwenyewe ameshangaa kuona picha hizo zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa ana uhusiano wa kimapenzi na Kusah, jambo ambalo halina ukweli wowote.

 

“Ni maneno tu ya watu wanaopenda kunizungumzia. Hivi inawezekana watu wakawa wananijua kuliko ninavyojijua mimi mwenyewe? Nimeshangaa kuona picha yangu na Kusah, eti mimi ninatoka naye kimapenzi.

 

“Jamani siyo kweli na sipendi watu wanavyonipakazia,” alisema Amber Lulu.

Stori: Neema Adrian, Dar

Toa comment