The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu, Makomando Wafunika Usiku wa Miss Kinondoni 2019 – Video

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’  (kulia) akiongea jambo na washiriki wa Miss Kinondoni.

USIKU wa kuamkia Julai 13, 2019, wasanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, Kundi la Makomando, Bi. Aisha na Wine walitoa shoo ya aina yake usiku wa kumtafuta Miss Kinondoni katika ukumbi wa Life Park Mwenge, ambapo mlimbwende Queen Mugesi Aynory (19) ameibuka kidedea na kuvaa taji lililokuwa linashikiliwa na Queen Elizabeth Makune.

Mshindi wa pili alikuwa Prisca Kisunda, wa tatu Leila Adim,  wa nne Queen Anthony na wa tano Flaviana Sreven.

Msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Bi. Aisha, akitumbuiza katika hafla ya Miss Kinondoni.
Kundi la Makomando,  Muki na Fredy, wakitoa burudani.
Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada, Wine,   akitoa burudani.

 

Comments are closed.