The House of Favourite Newspapers

VIDEO: JPM KUTOA 1.5 BIL. UJENZI HOSPITALI KATORO, BUSERESERE

 

Rais John Magufuli.

RAIS John Magufuli leo,  Julai 15, 2019, amewaahidi wananchi wa Kata ya Katoro, Buseresere, kuwapa Shi. bil. 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya eneo hilo.

 

Magufuli ameyasema hayo akiwa na njiani kwenda kuzindua nyumba 15 za makazi ya askari katika eneo la Magogo mkoani Geita ambapo amewapongeza pia kwa juhudi za kuleta maendeleo sehemu hiyo akiwaahidi pia kulitatua suala la ukosefu wa maji linalowakabili.

 

Pamoja na kupongeza juhudi za kufikisha umeme sehemu hiyo, rais amewataka viongozi wa sehemu hiyo  kukaa pamoja na kutatua  ni wapi hospitali hiyo ijengwe kwani kulikuwa na malumbano ya pande mbili kuhusu ni wapi ijengwe.

 

Amewataka pia wafanyabishara wa dhahabu kuuza madini hayo  katika masoko halali na si kwa madalali.

 

Vilevile, ameahidi kuwatafutia gari la polisi kwa ajili ya kuhudumia sehemu hiyo.

Comments are closed.